Tuesday, 17 March 2015
MAHAKAMA YAAMURU LIGI KUU KENYA IENDELEE .....>>
Mahakama kuu ya Kenya imeiruhusu kampuni inayoendesha ligi kuu ya Kandanda kuendelea mbele baada kutupa nje ombi la kuwasimamisha lililowasilishwa mahakamani na shirikisho la soka nchini Kenya FKF.
Ligi hiyo ya KPL msimu huu ilikuwa imesimamishwa kwa zaidi ya majuma matatu .
Jaji Lady Justice Roselyne Aburili alitupilia mbali amri ya mahakama kuu iliyotolewa tarehe 22 Februari na jaji Mbogholi Msagha.
Uamuzi huo uliibua vifijo shangwe na nderemo kutoka kwa mashabiki ndani na nje ya mahakama hiyo ya Milimani jijini Nairobi.
Afisa mkuu mtendaji wa KPL , Jack Oguda, ameiambia BBC kuwa wamefurahishwa sana na uamuzi wa mahakama na hivyo wanajiandaa kupanga upya ratiba kwa niya ya kufufua ligi hiyo kuanzia mwishoni mwa juma.
''hivi sasa tuko katika mkutano ambao tunajadili ratiba ya mechi,nina hakika timu zote zinapania kuendelea mbele la ligi na mashabiki wetu pia wanatarajia ligi iendelee mbele''alisema bwana Aguda.
Jaji Aburili alisema kuwa viongozi wa shirikisho hilo la FKF wanaweza kuendelea mbele na keshi kibinafsi kwani kulingana na sheria za nchi ya Kenya Vyama vya kijamii haviwezi kushtaki mahakamani.
Uamuzi huo hata hivyo uliwaacha wakereketwa wa kandanda nchini Kenya vinywa wazi kwani kuanzia sasa ligi ya KPL na ile iliyokuwa ikiendeshwa na shirikisho la soka FKF zitaendelea mbele bila kuhitlafiana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment