Mahakama nchini Misri imemhukumu
adhabu ya kifo kiongozi mwandamizi wa kundi la Muslim Brotherhood,
Mohamed Badie na wanachama wengine muhimu kumi na watatu wa kundi hilo
lililopigwa marufuku nchini humo.
Mahakama za Misri zimewahukumu mamia ya watu wanaotuhumiwa kuwa wafuasi wa kundi la Muslim Brotherhood adhabu ya kifo baada ya kesi zilizoendeshwa haraka haraka nakukosolewa na vikundi vya kutetea haki za binadamu na serikali za nje.
Muslim Brotherhood ilitangazwa kuwa kundi la kigaidi mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment