Mchezaji nyota wa Real Madrid ya
Uhispania na Ureno Christiano Ronaldo ndiye binadamu maarufu zaidi duniani
kwenye Facebook.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30
amempiku Mwanamuziki maarufu kwa kunengua kiuno Shakira nawafuasi zaidi ya
milioni 107.
Ronaldo anawafuasi 107,096,356
wakilinganishwa na 107,087,100 Shakira
Ronaldo aliweka rekodi kwa kuwa
mchezaji maarufu zaidi duniani alipotimiza wafuasi milioni 100 mwezi
Oktoba
mwaka uliopita.
Nyota huyo wa Real Madrid alijiunga
na mtandao wa kijamii wa Facebook mwaka wa 2009.
Na si hapo alikodhibitisha udedea
wake, Ronaldo anazaidi ya wafuasi milioni 34 katika mtandao wa kijamii wa
Twitter ambako anaorodheshwa katika nafasi ya 13.
Ronaldo anawafuasi 107,096,356
Msanii h Katy Perry ndiye
anayeongoza kwa umaarufu kwenye twitter akiwa na jumla ya wafuasi milioni 66.6.
Justin Bieber, Barack Obama, Taylor
Swift, YouTube, Lady Gaga, Justin Timberlake, Rihanna, Britney Spears, Ellen
DeGeneres, Instagram na Twitter ndio wanaompiku Ronaldo.
Licha ya hiyo yeye ndiye mwanaspoti
maarufu zaidi kwenye mtandao huo wa Twitter.
Mshambulizi wa Brazil na Orlando
City Kaka ndiye mchezaji wa pili kwa umaarufu akiwa na wafuasi milioni 22.2
million.
Ronaldo ndiye mchezaji maarufu zaidi
duniani
Licha ya kuwa maarufu na wafuasi wa
timu ya Uingereza ya Manchester United kiungo machachari Wayne Rooney
anashikilia nafasi ya 95 katika mtandao huo akiwa na wafuasi milioni 10.8
million.
Katika Facebook hata hivyo, Mchezaji
bora mara nne duniani na Mshambulizi wa Barcelona ,Lionel Messi ndiye
mwanaspoti wa pili kwa umaarufu duniani.
Messi anawafuasi milioni 78.
Orodha
ya Facebook
1. Facebook for Every Phone
|
544 milioni
|
2. Facebook
|
170m
|
3. Facebook Sales Germany
|
170m
|
4. Ronaldo
|
107m
|
5. Shakira
|
107m
|
6. Eminem
|
98m
|
7. Vin Diesel
|
90m
|
8. Rihanna
|
89m
|
9. YouTube
|
86m
|
10. Barcelona
|
83m
|
11. Real Madrid
|
82m
|
12. Michael Jackson
|
80m
|
13. Lionel Messi
|
78m
|
14. Justin Bieber
|
77m
|
15. Katy Perry
|
77m
|
16. Bob Marley
|
76m
|
17. Harry Potter and the Deathly
Hallows
|
76m
|
18. Will Smith
|
76m
|
19. The Simpsons
|
74m
|
20. Taylor Swift
|
74m
|
Nyota wa zamani wa England David
Beckham anafunga orodha ya tatu bora kwa wafuasi milioni 52 .
No comments:
Post a Comment