Thursday, 19 March 2015

TUTOKE VIPI ? INATOA WABUNGE ... HAWA NI WAWILI TU >>

Katika harakati za kutafuta nafasi za uongozi wa kitaifa , Rais wa jamhuri ya muungano na mwenyekiti taifa ccm J. KIKWETE alisisitiza vijana wajitokeze kwa wingi .. nafikiri ni kwa ukweli kua vijana ndio nchi yao hii leo .

TUTOKE VIPI? inao vijana kadhaa ambao tungependa muwajue , ni vijana kutoka kundi la TUTOKE VIPI ? ambao wamemua kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbali mbali za uongozi nchini , hii ni faraja kubwa sana kwetu kwa kua hawa tanaamini kua watatuwakilisha vizuri kwakua wameweza kuchanganya siasa na ukweli , na pia tumewapika ki ukweli wajue wakizengua wasirudi majimboni hata kusalimia coz ni vijana wetu na tutawaadhibu .

Kwa kifupi ndugu zangu niwalete machoni penu wanangu , watoto wetu wana TUTOKE VIPI ? waliokwisha jionyesha kua tayari kugombea uongozi wa juu ki serekali ili watupigie kelele bungeni wakati wa kudai maendeleo ya , biashara kitaifa , viwanda , KILIMO , na Elimu kwa vijana .

Tunataka watau kama hawa kwa wingi waende huko bungeni , wapige kelele dunia ijue hali yetu , taifa litusikilize , lituhangaikie kwa kua maisha yetu vijana wa Tanzania kwa sasa hatuna dira , na ni lazima ipatikane with no time coz we wstd lng time and now we have non .



ESTER CHARLES MAMBALI : huyu ni mwanaharakati toka chama cha mapinduzi wa ngazi ya ujumbe wa baraza ila pia mwenyeuelewa mkubwa wa IKULU ya Tanzania kwakua ni mwanaharakati mtetezi wa vujana aliyeijua ikulu kwa kujitetea na kutetea TAIFA LA VIJANA .

Huyu ESTER ameingia kwenye mbinje za kutafuta kuongoza vijana toka mwaka 2002 na ameweza kufanikiwa mwaka 2012 kupata ujumbe wa baraza TAIFA nafasi ya juu sana , (jana nimepata msg nyingi sana whtsup kumhusu huyu manzi ...,, wana eeh! huyu beibe ana mtu wake na wanapendana tusimpe ma nyang'au test akafeli ndoa akapoteza kiti huko Kilimanjaro ambapo anaenda kupambana kupata nafasi ya ubunge viti maalumu .

nilifurahi kujua ESTER anakwenda Kilimanjaro , ni kamanda yule japo yuko ccm , namuombea kwa mungu achukue kiti tukawakilishe vijana bungeni , mimi mke wangu anatokea kaskazini huko huko tena moshi ..(kicheko) nitahakikisha anapata kura ya mke wangu na wengine ninaowajua .. hayo yalikua maneno ya kamanda mmoja ngazi ya juu kutoka makamanda wetu gwandani CHADEMA.

Ndugu zangu tunae mwanaume kamanda  ..: VICTOR BHWANA anaekwenda kuomba ridhaa ya masela na wazee wa shinyanga kupitia chadema ..




nisikilize mwanangu huyu msela ni miongoni mwa masela waliojihangaikia wenyewe kwa kujitafutia na kujihudumia wenyewe , hii ni aina ya watu tunaoweza kuwaamini kwakua wanatoka katika mzazingira halisi tunayotoka vijana na wana ma idea ya kufa mtu sisi hatutaki pesa wala pombe zao .. tunataka wakiingia pale wawakilishe mawazo na michongo ya manufaa kwa vijana ili tusonge mbele ..

Anataja kua kwa sasa anakwenda kupambana kule SHINYANGA kupata ridhaa ya kikamanda toka kwa wana shinyanga ili awaletee maendeleo ya kisasa kwa wengi .

Tunamuunga mkono kwa dhati , VICTOR ni kijana mwenye mawazo mazuri , anajua pia ethics za uongozi all we need ni kuwaingiza vijana wa kutosha pale Dodoma ili kama rais atakua LOWASSA hawa vijana wampe changamoto jamaa atuletee miradi , viwanda , aboreshe elimu kwa uma , atupe elimu ya haki za kuishi na wajibu wetu , na mengine .

TUTAENDELEA SIKU NYINGINE .

No comments:

Post a Comment