Tuesday, 31 March 2015
LUDA na DRAKE .. 100 - 100 SASA
NYOTA wa Hip Hop nchini Marekani, Christopher Brian ‘Ludacris’ na mkali kutoka kundi la Young Money, Aubrey Drake, wamemaliza ugomvi wao wa miaka mitano.
“Binadamu hatujakamilika, mimi na Drake tulikuwa na mambo yetu, akiwa kama binadamu alikuja kwangu na kuomba msamaha tumeyamaliza.
“Tulikuwa na mgogoro kwa kipindi cha miaka mitano, halikuwa jambo zuri na ndio maana kila kitu kipo sawa kwa sasa.
“Vijana wengi hawapendi kukubali kosa, lakini mtu mwenye akili timamu anatakiwa kukubali na kuchukua hatua,” Alisema Ludacris.
Chanzo cha ugomvi wao hakukiweka wazi huku akiwataka mashabiki wao kusubiri wimbo wao walioshirikiana
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment