Tuesday, 17 March 2015
Kimenuka Siwena na Nay wa Mitego, Nay Afunguka ' Sina Mke Sijaoa na sina mahusiano ya kimapenzi na Mwanamke yoyote Yule'
Msaniii Emmanuel Elibarick alimaarufu kama Mr Nay ameonesha dalili ya wazi kuwa hana mpango tena wa kuwa katika mahusiano na Mchumba wake huyo Siwema ambaye amezaa nae mtoto wa kiume aitwae Curtis miezi kadhaa iliyopita.
Kupitia ukurasa wake wa Instgram Nay wa mitego siku mbili zilizopita aliweka post ambayo ilikuwa inasema kuwa kwa sasa ana watoto watatu na ana mapenzi ya kweli na watoto wake lakini hana mpango wala hana mahusiano ya kimapenzi na mama wa watoto wake hao bali anawaheshimu wanawake hao kama wazazi wenzake.
"Mr_Nay Baba wa watoto watatu... Sina Mke I mean Sijaoa na sina mahusiano ya kimapenzi na Mwanamke yoyote Yule... Kati ya niliozaa nao. Nawapenda watoto wangu nawaheshim mama zao..SingleBoy am in love with my son and daughters... Rishma, Curtis na Munie"
Kwa upande wake Siwema ambaye ni mama wa Mtoto wa Nay juzi aliweka picha ya Mzazi mwenzake na kuwataka mashabiki zake wafunguke lolote juu ya picha ile ila Comment nyingi zilionesha kuwa watu hao hawapo sawa au hawapo pamoja kwa sasa kama ambavyo baadhi zinasema.
"kaysamira: Siwema Mimi nakupenda siwez kukujudge chochote sababu mapenzi upofu namuomba Mungu akupe jicho la tatu na uweze kusonga mbele,mambo kama hayo hutokea na yanapita na kama yeye hakutaki usijali kuna wanaume wengi tu wanaopenda kuwa na mtu kama wewe tena wazuri kuliko yeye labda ndio chance mungu kawapa ili uweze kukutana na prince charm wako lakini kama umeandikiwa kuwa na baba Curtis hakuna mwenye kupinga hilo lakini aache kuwadhalilisha na kutumia udhaifu wenu kama mwanamke inauma anachezea sana hisia zenu"
"Augustinasimon37: Hakuna wa kumjudge mtu hapa, mapenzi ni ya wawili tu. kabla hakuzaa walikuwa sawa wakipendana iweje sasa ndio maana tunaumia, tunawaombea wasiachane, kibinadam sio vizuri. Nakupenda bure Siwema mpende mtoto wako ndio kila kitu kwako"
Lakini pia Nay wa Mitego leo amepost picha akitoka Mwanza huku akiwa na Mwanae Curtis akimnywesha Maziwa ya kopo hali ambayo inaonyesha wazi kuwa huenda mtoto huyo yupo chini ya himaya ya baba na si mama tena kitu ambacho kinaweza kutoa majibu ya wazi kuwa watu hao huenda wameachana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment