Saturday, 14 March 2015

CHELSEA ITASHINDA LIGI .. MOURINHO ...>>


 
 
Kilabu ya Chelsea itashinda ligi ya Uingereza,kocha wa kilabu hiyo Jose Mourinho amebashiri.
The Blues waliondolewa katika mashindano ya kilabu bingwa barani Ulaya na kilabu ya Parsi St Germain katika mechi ya katikati ya wiki lakini bado inaongoza jedwali la ligi ya EPL ikiwa na pointi tano huku ikiwa zimesalia mechi 11.

Mournho:Timu iliong'atuliwa katika mashindano ya kilabu bingwa barani ulaya ni timu ile ile inayoendelea kuongoza ligi ya Uingereza tangu siku ya kwanza.

''Ni wachezaji wale wale walioshinda kombe la capital One Cup na wachezaji haohao ndio watakaoshinda ligi ya EPL''.alisema kocha huyo.

No comments:

Post a Comment