Duru za mahakama ya Misri zinasema
kuwa mahakimu kama 40 wamelazimishwa kustaafu - inavoelekea kwa sababu
wanaonekana kuwa wanaunga mkono Muslim Brotherhood.
Wengine walijiunga na kundi lilounga mkono Brotherhood kabla ya Rais Morsi kutolewa madarakani.
Sheria ya Misri inakataza majaji kujihusisha na siasa, lakini wanaharakati wanaotetea haki za kibinaadamu wanasema wakuu hawasemi kitu kuhusu wale mahakimu ambao wazi wanamuunga mkono rais wa sasa wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi.
No comments:
Post a Comment