Wednesday, 11 March 2015

TUTOKE VIPI NI NINI ... ?? MALENGO YAKE NI YAPI ??




HABARI ..! 

Najua kwa muda sasa utakua umejiuliza hii tutoke vipi ni nini ? na kazi yake nini ?

Na miongoni mwa vitu vilivyokuja kichwani kwako ni kua hii ni blog ... YES ! ni blog ni sawa upo sahihi .. .

TUTOKE VIPI ? ni zaidi ya BLOG , hii ni harakati ndogo ya vijana wa kitanzania wenye maisha ya kukata tamaa na watafutaji waliopo gizani .

Tunalo kundi kubwa sana la vijana kwenye nchi yetu , tumesikia kua kufikia 2023 tutakua tumefika milioni 60 ., hawa ni watu wengi sana ikiwa hawana mwelekeo na ni wachache kama taifa likiweka dira ya kueleweka .

TUTOKE VIPI ? inaunganisha vijana kupita starehe , makongamano , vipindi vya radio na TV , wanamuziki , waigizaji na watu maarufu nchini Tanzania .

TUTOKE VIPI ?  imeanzishwa na mimi ( pichani ) jina langu MIKAEL CODE 1 * na tupo kama nane hivi vijana wa mjini wenye ruhusa za ubongo kufikiri .

TUTOKE VIPI ? tuna umri wa miezi miwili ya kiutendaji kwa maana ya mandalizi baada ya wazo , na nyuma ya hapo tulipoteza kama wiki mbili hivi kupata jina na kuangalia namna ya kulinda sheria za nchi na katiba ya jamhuri ya muungano .

Tulipitia kwa kina RESULT (matokeo ya jitihada zetu ) kutoka serekalini na tiliafikiana yafuatayo :
 A) Tulijua fika kwa hali ilivyo sasa kuna ulazima vijana tujitokeze kutetea vijana wenzetu ambao ndio taifa kwa sasa , na kwamba changamoto kubwa tutaipata kwa serekali kwakua kila tutapofanya jambo la kumsaidia kijana tutakua tunaiumiza serekali  .

B) Tuliamua kwa pamoja kufanya mambo ambayo yangeleta changamoto kwa jamii na bila kuiathiri serekali ambayo hatukutaka kuingia uadui nayo kutokana ukweli kua ile ni serekali , hivyo basi tukaanza kwa kujua matatizo sugu ya vijana , njia za kuyatatua na pia kuaandaa mpango burudani kuzunguka mikoa mikubwa ya nchi yetu kutangaza jina letu na kuhamasisha vijana .

Tusifurahishwe na wingi wa watotowadogo wa shule za msingi madarasani na kuutizama mpango wa kuwapa elimu tu . haina maana .. nitakwambia kwanini .

Huyu mtoto tunaempa elimu mazingira anayoishi na mzazi au wazazi yako vipi ? baba wa huyu mtoto hajulikani alipo na mama anafanya kazi ya kugonga kokoto na amempeleka mtoto shule ili na yeye apate muda wa kufanya kazi wapate mlo japo wa siku ok ? jiulize haya malezi yatamfanya huyu mtoto kuja kua nani ??? 

muda huo kumbuka na watoto wa mitaani wanaongezeka kila saa moja nao pia ni vijana wajao wa Tanzania na wapo kwenye lile kundi la watu milioni 60 .


Hii maana yake nini ? vijana wa wakati huu tuliopo weengi hawana vyanzo vyovyote vya mapato au  jambo linalowaandalia kesho yao .. kwa hivyo wanakaa bila kitu cha kufanya kwa muda mrefu sana , na from that now fikra PEVU zinaanza ... BURUDANI na hapo kwa kua hawana pesa burudani pia ni ya kimasikini KIROBA ,NGONO .. sasa jiulize hata buku ya CON.. hana hapo ni mtoto au MARADHI huyu bado ni kijana mtanzania .



kwa sababu hizi na za mapenzi kwa taifa letu tukaamua yakwamba sisi tutakua mfano kwa kuhamasisha vijana pamoja na serekali wajue hatari inayotukabili na jinsi ya kuitatua .

TUNAZO MBINU KADHA WA KADHA za namna ya kudhibiti au kupunguza matatizo ya vijana hapa tanzania . (hatuwezi kuweka hadharani ) ila kwenye sekta mbalimbali za vijana TUNAYO MAJIBU .




MALENGO YA TUTOKE VIPI ? 

Tunakusudia katika uchaguzu huu wa mwaka huu 2015 tutaweza kushawishi na kuamsha ari za vijana walio wengi  kufanya yafuatayo : KUJITOKEZA KWA WINGI WA AJABU KUPIGA KURA 
                                         KUCHAGUA MGOMBEA SAHIHI 
                                         KUIKIMBUSHA SEREKALI MPYA UWEPO WETU VIJANA NA UWEZO WETU ILI KUTUPA KIPAUMBELE TUNACHO STAHILI .
                                        KULETA UMOJA WA KITAIFA .

Haya ni malengo mapana ki ufafanuzi ila malengo makuu ni mawili .. 1) KUUNGANISHA VIJANA 2) KUUTUMIA UMOJA HUO KUTATUA CHANGAMOTO ZA KI MAISHA ZA VIJANA .

TUNALENGA KUANDAA MPANGO WA TAIFA KUHUSU VIJANA NA KIPATO 
TUNALENGA KUISHAWISHI SEREKALI KUPUNGUZA UAGIZAJI ILI KUTENGENEZA HITAJI LA NDANI KWA KUANZIA ...


 



NITAENDELA . .. 

NATOA POLE KWA WALIOFIKWA NA AJALI LEO HII HUKO IRINGA MUNGU ALITOA MUNGU AMETWAA .





No comments:

Post a Comment