Vituo vya kupiga kura vilifungwa Jumapili magharibi nchini Ethopia
baada ya uchaguzi wa kwanza wa bunge kufanyika tangu kufariki kwa
kiongozi wa muda mrefu Meles Zenawi.
Wakosowaji wanasema ni machache yaliyobadilika tangu kufariki kwake na chama chake tawala kinatazamiwa kupata ushindi mkubwa.
Vyama vya upinzani vimelalamika kwamba wafuasi wao wamebughudhiwa na
serikali inaendelea kutumia mbinu za ukandamizaji na kuufanya uchaguzi
huo kutokua na mana.
Maelfu na maelfu ya wapigajikura walijitokeza tangu alfajiri mjini
Addis Abeba na kusimama kwa mistari mirefu katika vituo vya kupiga kura
katika shule, ukumbi wa umma na mahema katika mji mkuu wenye wakazi
milioni 3 unaokuwa kwa kasi.
Kwa karibu robo karne sasa tangu 1991 chama tawala cha Ethiopia
People’s Revolutionary Democratic Front EPRDF kimesimamia mageuzi ya
taifa hilo tangu lilipokua chini ya mfumo wa kikomunisti ambapo njaa na
umaskini ulikitiri, hadi kugeuka kuwa taifa linalowavutia wawekezaji wa
kigeni hii leo.
Kwa hivyo ni wazi mshindi wa uchaguzi wachambuzi wanasema anatazamiwa
kuwa ni EPRDF, kwani upinzani hautarajiwi kupata matokeo mazuri, kwani
katika uchaguzi wa mwisho wa bunge miaka mitano iliyopita vyama vya
upinzani vilipata ushindi wa kiti kimoja bungeni.
Na katika uchaguzi wa 2005 upinzani ulipata viti 147 lakini wengi wa
wabunge hao hawakushirikia katika vikao vya bunge wakidai kulikuwa na
wizi.
Matokeo ya awali ya uchaguzi wa Jumapili yanatazamiwa mnamo siku
chache zijazo huku matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa mwezi ujao.
No comments:
Post a Comment