Blair alimwandikia barua katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kuhusu kujiuzulu kwake na kuahidi kusaidia Jumuiya ya Kimataifa katika kazi zinazohusu Israel na Palestina katika siku zijazo.
Vyanzo vya habari vilivyokaribu na Blair vinasema, ataendelea kuwepo akijihusisha na baadhi ya shughuli na eneo hilo. Watoa habari hao wanasema kuwa waziri mkuu huyo wa zamani anaamini kuwa mtazamo mpya unahitajika.
Lakini wakosoaji wanasema Blair alipambana katika jukumu ambalo lilikuwa na mipaka katika maendeleo ya kiuchumi na ameshindwa kuleta matokeo chanya.
Ofisa mmoja wa Palestina amemlaumu Blair kwa kufanya kazi kwa upendeleo ili kuwaridhisha Waisrael na Marekani.
Kamati hiyo ya Umoja wa Kimataifa inaoshughulikia migogoro ya Mashariki ya Kati unaundwa na UN, EU nchi ya Marekani na Urusi.
No comments:
Post a Comment