VIBAKA ambao hawakufahamika mara moja mwishoni mwa wiki iliyopita, walivunja kioo kidogo cha gari la nyota wa Bongo Fleva, Khalid Ramadhan ‘Tunda Man’ na kumkomba vitu mbalimbali vikiwemo power window, kompyuta mpakato na fedha katika tukio lililotokea Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
“Nimelizwa, roho inauma sana wamechukua na pesa shilingi 35,000 ambazo zilikuwa juu ya dashbod, wamebakisha elfu tisa tu” alilalamika Tunda Man ambaye alisema tukio hilo liliripotiwa katika kituo cha Polisi Kigamboni.
No comments:
Post a Comment