Chris Brown na Nicki Minaj wote wanawania tuzo katika vipengele 6.
Nicki Minaj.
Katika kipengele cha video bora ya mwaka, Brown ametajwa mara mbili kwa video zake za Loyal na New Flame.Minaj naye yupo juu akitajwa katika vipengele sita kikiwemo cha video bora ya mwaka kwa wimbo wake wa Anaconda huku Beyonce na Lil Wayne wakifuatia kwa kutajwa katika vipengele vinne.
Brown pia ametajwa katika vipengele vya Mwanamuziki Bora wa Kiume wa R&B/Pop, Tuzo ya chaguo la watazamaji na akitajwa tena mara mbili katika vipengele vya Colabo bora kwa wimbo wake wa Loyal, aliomshirikisha Lil Wayne na Tyga, pamoja na wimbo wake wa New Flame, aliowashirikisha Usher na Rick Ross.
Chris Brown akiwa amembeba mwanaye.
Pia ametajwa mara mbili katika kipengele cha Tuzo ya chaguo la watazamaji kwa ngoma yake ya Only na kwenye ngoma ya Rae Sremmurd ya Throw Some Mo aliyoshirikishwa.
Beyoncé.
Tuzo hizo zitatolewa Juni 28, mwaka huu nchini Marekani.
No comments:
Post a Comment