Tuesday, 19 May 2015

VANESSA MDEE KUIWAKILISHA TANZANIA MKUTANO WA KIUCHUMI ....>>

VANESSA Mdee ni miongoni mwa wasanii tisa wa muziki kutoka nchi mbalimbali za Afrika, watakaowakilisha katika mkutano wa kiuchumi wa dunia kwa Afrika na wa viongozi wa nchi za Umoja wa Afrika wakati watakapozindua wimbo wa ‘Strong Girl’ unaohamasisha kampeni inayojulikana kama “Poverty is Sexist”.

Licha ya wimbo huo kuja kuzinduliwa rasmi katika mkutano huo utakaofanyika nchini Afrika Kusini, kwa sasa unaendelea kuzinduliwa katika nchi mbalimbali ikiwemo Nigeria, Msumbiji na Zimbabwe.


Wasanii wengine walioshiriki katika wimbo huo ni Victoria Kimani (Kenya), Judith Sephuma (Afrika Kusini), Waje (Nigeria), Arielle T (Gabon), Gabriela (Msumbiji) na Selomor Mtukudzi (Mtoto wa Oliver Mtukudzi wa Zimbabwe), Blessing Nwafor na Yemi Alade (Nigeria).
Vanessa alisema kampeni hii inawataka viongozi wa dunia kuwaweka wasichana mbele kwa mwaka huu 2015 kutokana na malengo mapya ya maendeleo yatakayoazimiwa na viongozi wa dunia katika Umoja wa Mataifa.

Alisema pia wimbo huo umeanza kuonekana sehemu mbalimbali ukiwa na ripoti ya kampeni ya ONE inayojulikana kama “Poverty is Sexist’ ikimaanisha umasikini unaaumiza zaidi jinsia moja.
“Ndani ya ripoti hiyo inaonyesha namna wasichana na wanawake wanavyotakiwa wawe na moyo wa mapambano ya umasikini uliokithiri huku ikionesha namna ambavyo wataweza kufungua fursa za uchumi kwa wanawake kunavyoweza kuwasaidia kwa jamii,’’ alisema.

Kampeni hiyo inaunga mkono wito wa viongozi wa dunia wa kupambana na ukosefu wa usawa wa kijinsia kwa kuwekeza zaidi kwa wanawake na wasichana ili kumaliza umasikini uliokithiri ifikapo 2030

No comments:

Post a Comment