Maafisa sita wa shirikisho la soka
duniani Fifa wamekamatwa katika hoteli moja mjini Zurich,Switzerland.
kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Watuhuhumiwa hao
ambao wanasemekana kuwa ni pamoja na makamu wa rais wa
Fifa,wanashikiliwa wakisubiri kusafirishwa kwenda Marekani.Shutma hizo zinahusisha rushwa ya takriban kiasi cha dola za Marekani milioni 100 kwa kipindi cha zaidi ya miaka 20
Wanachama wa Fifa wanakutana mjini Zurich kwa ajili ya mkutano wao wa mwaka siku ya ijumaa, ambapo rais wa Shirikisho hilo Sepp Blatter anawania muhula wa tano.
Mwana mfalme Ali Bin Al-Hussein wa Jordan,ambaye ndiye mpinzani pekee wa Blatter amesema tukio hilo ni "baya kwa maendeleo ya soka".
Gazeti la New York Times limesema askari kanzu walichukua funguo za chumba cha hoteli kutoka eneo la mapokezi ya hoteli ya Baur au Lac hotel ambayo maafisa hao walikuwa wakiishi na kuingia vyumbani mwao.Gazeti hilo limesema Operesheni hiyo ilifanyika kwa utulivu.
Jeffrey Webb, Mkuu wa shirikisho la Amerika ya Kaskazini na Kati na Visiwa vya Caribbean ametajwa kuwa mmoja kati ya maafisa waliokamatwa.
Maafisa wengine wa Fifa walishuhudiwa na BBC wakisindikizwa na Polisi kutoka kwenye hoteli hiyo ni:
Mkuu wa Shirikisho la soka la Costa Rica, Erduado Li, ambaye alikuwa akitarajia kuwepo kwenye mkutano wa kamati ya Fifa siku ya ijumaa.Wengine ni rais wa shirikisho la Uruguay Eugenio Figueredo,rais wa shirikisho la soka Amerika kusini Conmebol na wa Brazil,Jose Maria Marin,mwanakamati ndani ya Fifa,Polisi walionekana wamebeba mikoba yake kwenye mifuko ya Plastiki.
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni kwa vipi Blatter amekuwa Kiongozi wa Fifa kwa muda mrefu, pamoja na kuwepo kwa ripoti nyingi za vitendo vya rushwa lakini ameendelea kushikilia wadhifa huo.
Wizara ya sheria ya Uswiss imesema katika tamko lake siku ya jumatano kuwa maafisa wa serikali ya Marekani waliwashuku maafisa hao kupokea rushwa ya dola milioni 100, tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990 kwa ajili ya michuano ya Amerika ya kati.
Serikali ya Uswiss imesema itaidhinisha haraka kusafirishwa kwao.
Mwanzoni mwa mwezi huu, Blatter alisema anafahamu baadhi ya wafanyakazi wenzake wa zamani walikuwa wakichunguzwa lakini amekanusha kuwa uchunguzi
No comments:
Post a Comment