Polisi nchini Malaysia wanasema kuwa
wamepata karibu makaburi 140 na kile wanaamini kuwa ni kambi 28 haramu
za kuwasafirisha watu kimagendo karibu na mpaka na Thailand.
Aidha makaburi hayo yalitumiwa kuzika wahamiaji ambao walikufa wakiwa kizuizini.
Ugunduzi kama huo ulifanyika nchini Thailand yapata mwezi mmoja uliopita na kutibua operesheni kali dhidi ya walanguzi wa binadamu.
Oparesheni hiyo iliyoendeshwa na jeshi la wanamaji na polisi wa Thailand iliwaacha maelfu ya watu wakiwa wametelekezwa baharini ,na ikalazimu mashirika ya kupigania haki ya kibinadamu na wakimbizi kuingilia kati ilikuzishinikiza serikali za mataifa husika kuwaruhusu wahamiaji waliokuwa kwenye mashua hizo za wakimbizi kuweka nanga katika bandari zao.
Operesheni hiyo ilikuwa inawalenga walanguzi wa watu wa jamii ya waislamu wa Rohingya kutoka Myanmar na Bangladesh.
Waziri wa masuala ya ndani wa Malaysia aliviambia vyombo vya habari kuwa ameshangazwa kugundua kuwa huenda kambi hizo zimekuwa eneo hilo kwa miaka mitano.
No comments:
Post a Comment