Dogo akiwakomalia trafiki mpaka wananchi wakalazimika kuingilia kati.
Trafiki kwa msaada wa wananchi wakimtia pingu dogo huyo aliyekuwa akimpa kichapo mwenzake.
...Ilibidi itumike nguvu ya ziada kumtia pingu dogo huyo.
Mbali na kupigwa pingu bado dogo huyo aliendelea kuwakomalia trafiki.
...Dogo akitaka kuzipiga na afande mbali na kutiwa pingu.
Mwanza
KIJANA mmoja ambaye hakufahamika jina lake jioni hii amewahenyesha Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani jijini Mwanza walioingilia ugomvi uliokua ukimuhusisha kijana huyo na mwenzake katika eneo la Posta ya Zamani.
Tukio hilo limetokea majira ya saa 10:15 jioni wakati vijana wawili walipozichapa hivyo maofisa hao wa usalama barabarani kuamua kuingilia ugomvi ili kumuokoa kijana mmoja aliyoonekana kuzidiwa na mwenzake.
Tofauti na walivyofikiria, maafande hao walitolewa kijasho na dogo huyo aliyekuwa amemzidi ubavu mwenzake huku wakipata tabu wakati wakijaribu kumtia pingu ili wampeleke kituo cha polisi.
Mbali na kuwakomalia wanausalama hao, dogo huyo pia alikuwa akiwaporomoshea matusi wakati wakijaribu kumtia nguvuni hali iliyopelekea wananchi kuingilia kati kuwasaidia polisi kumtia pingu dogo huyo.
Baada ya ushirikiano wa wananchi, polisi walifanikiwa kumpiga pingu dogo huyo na kumpeleka Kituo cha Polisi Kati huku akila kichapo cha hapa na pale.
No comments:
Post a Comment