KABANG! Staa anayevuna fedha nyingi kupitia kipaji chake cha muziki, Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amewatelekeza watoto katika Shule ya East Africa International jijini Dar ambao aliahidi kuwalipia ada, Risasi Mchanganyiko linakuwa la kwanza kukudondoshea.
Wanafunzi wanaodaiwa kutelekezwa na Staa anayevuna fedha nyingi kupitia kipaji chake cha muziki, Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
“Jamani Diamond kila kukicha anafanya shoo za mamilioni lakini ameshindwa kuwalipia ada wale watoto ambao aliahidi kuwasomesha. Wamesoma mwaka mmoja tu, mwezi uliopita walitimuliwa na sasa wako nyumbani. Inauma sana kwani hawa watoto walitolewa kwenye shule za kawaida na yeye ndiyo akawapeleka kule,” kilisema chanzo hicho.
WAZAZI WANASEMAJE?
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa wazazi wa wanafunzi hao, Fadhili alisema watoto wao walitimuliwa shuleni tangu April mwaka huu kwa kuwa, Diamond hakuwahi kuwalipia ada tangu alipowaingiza pale.“Inauma sana, kwani tangu watoto wetu watimuliwe tumekuwa tukifuatilia kwa mtu tuliyeambiwa ni msimamizi wa Diamond (jina lake linahifadhiwa kwa sasa) lakini hatupi jibu la kueleweka.
“Tunaomba sana jamani, mtusaidie na nyie waandishi maana watoto wanapitwa na masomo na isitoshe kabla ya hapo walikuwa wakisoma kwenye shule za kawaida,” alisema mzazi huyo.
MSIKIE MWALIMU MKUU
Paparazi wetu alifunga safari mpaka shuleni hapo maeneo ya Mikocheni, Dar na kufanikiwa kuzungumza na Mwalimu Mkuu, Mercy Githirua ambapo alithibitisha watoto hao kusimamishwa masomo kutokana na kukosa ada.“Tulivumilia kwa muda mrefu sana kwani tulimwamini Diamond tukawapokea watoto hao na kuanza masomo. Siku aliyokuja kuwakabidhi hapa shuleni aliomba ‘invoice’ kwa ajili ya kututumia ada lakini yuko kimya mpaka leo.
“Sijapenda tabia ya Diamond, hivi anajua watoto wakimchukia itakuwa ni hatari sana kwake? Watoto wa watu walikuwa wanasoma huko akaenda kuwatoa na kuwaleta hapa lakini amewatelekeza, siyo vizuri kabisa,” alisema mwalimu mkuu huyo.
WANADAIWA SHILINGI NGAPI?
Kwa mujibu wa mwalimu mkuu huyo, watoto hao tangu walivyoingia Januari 21, 2014 hawakuwahi kulipiwa ada yoyote hivyo kila mmoja anadaiwa shilingi milioni moja na laki sita (1,600,000).
Staa anayevuna fedha nyingi kupitia kipaji chake cha muziki, Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
DIAMOND, MAMENEJA WAKE!
Juzi, gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Diamond kwa njia ya simu lakini ilikuwa imesetiwa kwamba inafanya kazi muda wote ‘bize’ hata alipotumiwa meseji hakujibu. Vivyo hivyo kwa mameneja wake, Fella na Bab Tale simu zao ziliita bila kupokelewa.
TUJIKUMBUSHE
Mwaka jana, Diamond aliandaa shindano la Nani Anaweza Kucheza Staili ya Wimbo wa Ngololo ambapo watoto kibao walijitokeza Leaders Club. Watoto hao wawili waliibuka kidedea kwa kuonesha uwezo mkubwa wa kucheza na ndipo zawadi yao aliamua kuwapeleka kwenye shule hiyo na kukutwa na yaliyowakuta!
No comments:
Post a Comment