Thursday, 28 May 2015

FIFA KIKAO CHA DHARURA ...>>>

Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA, Sepp Blatter, ameongoza kikao cha dharura cha wanakamati wakuu wa shirikisho hilo huko Zurich Uswisi.

Kikao hicho kinafuatia hatua ya kukamatwa kwa maafisa 7 wakuu na polisi huko Zurich Uswisi kwa tuhuma za ufisadi.

Blatter anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu uongozi wa FIFA.

Hata hivyo FIFA inasema kuwa kura za kumchagua rais mpya zilizoratibiwa kufanyika kesho zitaendelea mbele.

 
 
Mfumo wa utawala wa shirikisho la soka duniani FIFA
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amemtaka Blatter ajiuzulu.
Hata hivyo rais wa Urusi Vladimir Putin amemuunga mkono bwana Blatter akisema bila shaka hizo ni njama za Marekani za kumtaka Blatter asiwanie tena uongozi wa FIFA.

Wakati huohuo Mmoja ya wafadhili wakuu wa kombe la dunia anasema kuwa huenda akalazimika kutathmini upya ufadhili wake kwa FIFA ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa kurejesha hadhi ya mchezo wa kandanda.

Taarifa kutoka kwa kampuni ya VISA inatolewa kufuatia visa vya kukamatwa kwa maafisa 7 wa vyeo vya juu wa FIFA kwa madai ya ulaji rushwa.

 
Blatter anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu uongozi wa FIFA.
Wafadhili wengine nao wametoa maoni yao.

Kampuni ya Coca-Cola ilisema kuwa madai hayo yamechafua hadhi ya kombe la dunia huku kampuni ya magari ya Hyundai ikisema ina wasiwasi wa kesi zinazowaandama maafisa wa FIFA.

Blatter anawania muhula wake wa tano kama rais wa FIFA katika uchaguzi ulioratibiwa kufanyika hapo kesho.

 

No comments:

Post a Comment