Wanamgambo wanaoiunga mkono serikali
ya Iraq wa kishia wametangaza kuanzisha mapambano ya kuwaondoa
wanamgambo wa dola ya kiislam wa Islamic State nje ya mkoa wa Anbar.
Hii
inafuatia wanamgambo wa IS kuudhibiti mji mkuu wa Ramadi.Wanamgambo
wanaoiunga mkono serikali na vikosi vya jeshi wamekuwa wakirejea nyuma
katika mapigano hayo ya kutaka kurejesha mji mikononi mwa majeshi ya
serikali,na sasa kuna taarifa za makabiliano makali upande wa kusini na
Magharibi mwa mji wa Ramadi.
No comments:
Post a Comment