Rais wa Poland Bronislaw Komorowski amekubali kushindwa katika uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita.
Hata hivyo matokeo rasmi
yatatolewa japo kuwa matokeo ya awali yanaonyesha kwamba Komorowski
ambaye ni mshirika wa serikali ya mlengo wa kulia, ameshindwa kwa
asilimia 53 kwa asilimia arobain na dhidi ya mpinzani wake Andrzej Duda.Matokeo haya hayakutegemewa kwa Komorowski na yana chukuliwa kama tahadhari kwa serikali hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi wa wabunge baadae mwaka huu.
Poland imekuwa na uchumi imara katika miaka ya hivi karibuni ljapo kuwa wadadisi wa mambo wanasema raia wa taifa hilo wanadai kutonufaika na maendeleo hayo. Rais mpya wa Poland anatarajiwa kuanza kazi August mwaka huu.
No comments:
Post a Comment