Maafisa wa usalama wa Uswisi wanasema wanawashikilia maafisa kadhaa
wa vyeo vya juu ya Shirikisho la Kimataifa la Kandanda FIFA kwa tuhuma
za ulaji rushwa na kupokea hongo na baadhi yao watasafirishwa hadi
Marekani.
Gazeti la New York Times likiripoti juu ya tukio hilo linaeleza
kwamba maafisa wa usalama walova mavazi ya kiraia waliwasili katika
hoteli ya Baur au Lac alfajiri Jumatano, na kuchukua ufunguo wa baadhi
ya vyumba vya maafisa hao na kuelekea katika vyumba vyao.
New York Times likiwanukua maafisa wa usalama wa Uswisi wasotaka
kutajwa, inaripoti kwamba serikali kuu ya Marekani inawashitaki maafisa
hao kwa ubadhirifu wa mali, kuhalalisha fedha zilziopatikana kwa njia
zisizo halali katika kipindi cha miaka 20 hadi leo.
Maafisa hao walokamatwa wamefika Zurich kuhudhuria mkutano mkuu wa
FIFA ambao unatazamiwa kumchagua tena Sepp Blatter ambae anakabiliwa na
upinzani kutoka kwa mwana mfalme wa jordan Ali Bin Al Hussein hapo
Ijuma.
No comments:
Post a Comment