Sunday, 24 May 2015

JOKATE MWENGELO '' aka KIDOTI AMLIPUA DIMOND ...!

Jino kwa jino! Sexy lady anayefanya poa na ngoma yake ya Leo Leo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, amemlipua aliyewahi kuwa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye hivi karibuni alimwita makombo baada ya kusikia kwa sasa anatoka kimalovee na msanii Ali Kiba.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’

Akizungumza na gazeti namba moja la mastaa Bongo, Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Jokate alisema alishangazwa na maneno hayo ambayo hakustahili kuyatamka kwani kama ni ishu ya mtu kula makombo mbona hata yeye ni makombo na bado anakula makombo?

Jokate Mwegelo ‘Kidoti’

“Sijapendezwa na kauli ya Diamond na namshangaa sana, sijajua nini kimemkuta maana mimi sijamtaka wala hakuna ambapo niliwahi kumwambia kuwa ninatoka  au ninamtaka Kiba, zaidi ya maneno ya watu kwenye mitandao ya kijamii.

“Hata kama hilo lipo, bado sioni maana ya neno makombo kwani hata yeye ni makombo na anakula makombo kwa Zari (Zarinah Hassan) kwani nani asiyejua?” alihoji Jokate akionekana kuchukizwa na kauli hiyo ya Diamond na kuongeza:

“Yawezekana labda maana ya neno hilo hatulijui ndiyo maana tunalisema bila kuliangalia kwa umbali zaidi, hivyo ninachoweza kukisema ni kwamba mimi sijawahi kumtaka wala kumhitaji hivyo sioni kabisa sababu ya msingi ya kusema hivyo labda kama alikuwa na maana nyingine tofauti na hiyo.”

No comments:

Post a Comment