Zaidi ya watu milioni moja kutoka
nchini Brazil wameandamana dhidi ya rais wa nchi hiyo Dilma Rousseff,
huku wengi wao wakitaka rais huyo afunguliwe mashtaka ya ufisadi mkubwa
uliofanyika katika shirika la mafuta la serikali, Petrobras.
Maandamano makubwa kabisa yamefanyika katika mji wa Sao Paulo ambalo ni eneo la upinzani waliokuwa wakipita mitaani.
Mmoja wa waandamanaji Francisco Pestana alilalama akisema"Dilma hana uwezo wa kuongoza nchi yetu. Tunachokabiliwa nacho ni bahati mbaya sana, namna mamabo yanavyokwenda, yanaweza kuelekea kubaya zaidi, tutakuwa Venezuela nyingine."
Naye mwandamanaji mwingine mwanamke Janaina Lima anasema "leo ni maandamano ya watu. Watu wamejitokeza mtaani kusema hakuna ghasia zaidi, hakuna rushwa, hakuna uvivu zaidi, hakuna uzembe zaidi, hakuna utawala mbaya. Na kuunga mkono Brazil mpya."
No comments:
Post a Comment