Waandishi wa habari wa kigeni,
wanadiplomasia, wanaharakati na wasanii mbalimbali wametiwa mbaroni na
polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, wakiwemo waandishi wa
habari wa BBC.
Mwandishi wa BBC Maud Jullien anaripoti kuwa wanaharakati kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Senegal na Burkina Faso walikuwa na mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kinshasa unaohusu kuundwa kwa jukwaa jipya la kijamii la vijana wa Congo.
Hapo ndipo walipokamatwa na kupelekwa makao ya usalama wa taifa.
Waandishi wa BBC ni miongoni mwa waliokamatwa na wanasema wamewaona polisi wakiwapiga baadhi ya wanaharakati kwa kutumia marungu.
Lambert Mende ambaye ni msemaji wa serikali ya Congo amesema mkutano huo haukuwa halali na kusema kuwa raia waliokamatwa kutoka Senegal na Burkina Faso ni wachochezi hatari kwa usalama wa taifa la Congo.
Nchi ya Burkina Faso na Senegal zote zilikuwa na vuguvugu dhidi ya marais wao walipojaribu kubaki madarakani baada ya muda unaoruhusiwa kwa mujibu wa katiba ya nchi zao kumalizika.
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemkrasi ya Congo atakamilisha muhula wake wa mwisho ifikapo Januari, 2016.
Watu zaidi ya arobaini wameuawa katika vurugu zilizosababishwa na muswada wa uchaguzi ambao ungemuongezea muda wa kukaa madarakani.bert MendeCOngo
No comments:
Post a Comment