Sunday, 15 March 2015

WAHAMIAJI 64 KUTOKA ETHOPIA WAKAMATWA ....


Polisi mkoa wa Dodoma nchini Tanzania wanawashikilia wahamiaji haram 64 raia wa Ethiopia, huku mmoja wao akipatikana akiwa amekufa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma amenukuliwa akisema wanamshikilia dereva wa gari lililokuwa limewabeba watu hao ambao inaaminika walikuwa njiani kuelekea kusini mwa Afrika.

Hii si mara ya kwanza kwa wahamiaji wa aina hiyo kukamatwa katika mazingira hayo.
Mwaka 2012 watu 42 kutoka Eritrea walikutwa wamekufa katika lori mkoa wa Dodoma kwa kile kinachosemekana ni kukosa hewa kutokana na kufichwa ndani ya lori hilo.

No comments:

Post a Comment