Sunday, 15 March 2015

TUTOKE VIPI ? MACHINGA WACHANGISHA MKWANJA KUMTOA LOWASSA ... YES!


 

*Wamtaka Atangaze Nia,Agombee Urais Awamu Ya Tano.
*Wasema Sasa Ni Wakati Wa Matumaini Mapya Wakiamini Edward Ndio Mtu Pekee Wa Kutegua Bomu La Ajira

Umoja Wa Wafanya Biashara Wadogo Wadogo Nchini Almaarufu Machinga Kupitia Umoja Wao Wa Wamachinga Tanzania SHIUMA ~ TZ Wamefunga Safari Kutoka Makao Makuu Ya Shirika Hilo Mkoani Mwanza Mpaka Arusha Wilaya Ya Monduli Kumuomba Mzee Edward Ngoyai Lowassa Atangaze Nia.

Akisoma Tamko Lao Mwenyekiti Wa Umoja Huo Bwana Tatendo Alisema " Madhumuni Ya Safari Yetu Kwako Mh Edward Ngoyai Lowassa.

Kwa Nia Thabiti Na Dhamira Njema Kabisa Sisi Kama Jamii ya Watu Watanzania Tumepata Msukumo Wa kweli Na Dhati kuja hapa na Kukuomba Ndugu Yetu Kiongozi Wetu Ugombee Nafasi Ya Urais Katika Uchaguzi Mkuu Wa Urais.

Umoja Wa wamachinga tanzania Shiuma~Tz bila Ya Shinikizo lolote kwa maslai mapana ya taifa letu tumekaa na kufikiri kwa kina ikiwa ni pamoja na kufanya tathimini juu ya mustakabali wa taifa letu katika uchaguzi ujao, Tumejiridhisha wewe ndio Mtu sahihi kumpokea majukumu ya kuliongoza taifa hili ndugu jakaya mrisho kikwete katika awamu ijayo awamu ya Tano.

Tumejiridhisha juu ya Uwezo wako ndani ya chama na katika serekali, utumishi wako uliotukuka, uwajibikaji na uzalendo wako kwa taifa hususani katika kuona unawakomboa watanzania na kuondoa umasikini.

Kwa sababu hizo tumeshawishika kuja na maombi matatu

1.Kukuomba ufikirie kugombea uraisi kama hukuwa na nia hiyo

2.Utangaze nia ya kugombea urais

3.Uchukue form endapo mchakato huo utaruhusiwa rasmi kupitia chama chako.

Kwa kuwekea mkazo zaidi katika hilo hapa tumeambatana na kiasi cha pesa kitakachosaidia katika gharama za kuchuku form ya urais.

Rai yetu Kwa Watanzania Sisi kama wakazi wa mkoa wa nwanza na umoja wa wafanya biashara wa machinga tanzania, Tunawaomba watanzania wenzetu nchini kote kuhakikisha tunakuwa wamoja katika safari hii ya matumaini mapya kwa watanzania.

Mungu Mbariki Lowassa Mungu Tubari Wamachinga Tanzania Na Mungu Ibariki Tanzani"

Ombi Hilo kwa Mh Lowassa Ni Sehemu Ya Mavuguvugu Ya Nguvu Ya Umma Inayomtaka Mh Edward Lowassa Kugombea Uraisi Kupitia Ticket Ya Chama Hicho, Vijana Hao Wa Kitanza Kutoka Mikoa Kumi Inayounda Umoja Huo Wa Machinga Tanzania Wameweka wazi msimamo wao kwa sasa ni kupata kiongozi mwenye utayari wa kumaliza changamoto zao.

Akizungumzia Tamko Na Ombi Hilo Mh Edward Ngoyai Lowassa Mbunge Na Mjumbe Wa Halmashauri Kuu Kutoka Wilaya Ya Monduli Alisema Kwa Sasa Hana Cha Kusema Zaidi Anawataka Watanzania Wasubiri Utaratibu Kutoka Katika Chama Chake Cha Mapinduzi Utakapo mruhusu Kufanya Hivyo.

No comments:

Post a Comment