MKULIMA mmoja mkazi wa Kijiji cha Mlima kilichopo Kata ya Mwakijembe,
wilayani Mkinga, Mkoa wa Tanga, Silyvester Msubari, amefariki dunia
baada ya kuliwa na simba.
Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Mboni Mgaza, alisema jana kuwa mkulima huyo
aliuawa juzi alfajiri wakati alipokuwa shambani kwake akilinda mazao
yake yasiharibiwe na wanyama.
“Siku ya tukio, marehemu alikuwa shambani kwake akilinda mazao yake yasiharibiwe na wanyama.
“Wanyama hao wamekuwa wakizagaa mashambani kwa sababu Kata ya Mwakijembe
inapakana na Hifadhi ya Mkomazi yenye wanyama mbalimbali.
“Kwa hiyo nawaomba wananchi wawe na tahadhari muda wote pindi
wanapokwenda mashambani kulinda mazao yao ili wanyama wakali
wasiwadhuru.
“Ikibidi wananchi wawe katika makundi ili wanyama wakali wakiwavamia iwe
rahisi kwao kukabiliana nao vinginevyo watazidi kupoteza maisha,”
alisema Mgaza.
No comments:
Post a Comment