Kauli hiyo aliitoa wakati akihutubia kwenye
sherehe za Siku ya wafanyakazi Duniani zilizofanyika kitaifa mkoani hapa
kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Rais alikuwa akijibu hoja kadhaa zilizokuwapo
kwenye risala ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta)iliyosomwa
na katibu wake mkuu, Nicholaus Mgaya ambayo ilitaja madaio hayo,
yakiwamo ya kuongeza kima cha chini cha mshahara hadi kufikia Sh315,000,
kupunguza kodi ya malipo kadri unavyopata na kuundwa kwa Tume ya
Usuluhishi.
“Tuna madai 11 ambayo ni kima cha chini cha
mishahara, maboresho ya pensheni, makato ya kodi, Tume ya Usuluhishi
ambayo bado ina changamoto kubwa kwani sheria inasema suluhisho kati ya
mwajiri na wafanyakazi linatakiwa kufanyiwa kazi ndani ya siku 30,
lakini kwa sasa inafikia mwaka mmoja, na uhuru wa kujiunga kwenye vyama
vya wafanyakazi na mengine ambayo ni changamoto kwa wafanyakazi.
Tunaomba utusaidie kuyatafutia ufumbuzi,” alisema Mgaya katika risala
hiyo.
Lakini, Rais Kikwete, ambaye jana alizungumza
akichanganya na utani, alisema changamoto za wafanyakazi amezikuta na
haziwezi kumalizika, hivyo anamwachia Rais ajaye azishughulikie.
“(Rais wa Serikali ya Awamu ya Kwanza) Mwalimu
Julius Nyerere kwa miaka 27 alishindwa kuzimaliza (changamoto za
wafanyakazi). Rais wa awamu ya Pili, All Hassan Mwinyi hakuzimaliza,
Rais wa awamu tatu Benjamini Mkapa hakuzimaliza, na mimi siwezi
kuzimaliza. Hivyo zitakazobaki nikitoka madarakani, ninamwachia Rais
ajaye azishughulike,” alisema Kikwete.
Wakati wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Kwanza
na ya Pili, wafanyakazi walikuwa wakitarajia kusikia nyongeza ya
mishahara kutoka kwa Rais kwenye sherehe za Mei Mosi, lakini Mkapa
akaondoa utamaduni huo baada ya kueleza waziwazi kwenye moja ya sherehe
hizo kuwa Serikali itaongeza mshahara kama watu watachapa kazi.
Kikwete alitumia muda mwingi wa hotuba yake kuaga
na akaeleza kuwa hana mpango wa kuongeza muda kama baadhi ya wanasiasa
wanavyodai.
“Nawashangaa wanaodai kuwa Serikali ina mpango wa
kuongeza muda wa urais, kwani sina mpango wa kufanya hivyo,” aliongeza
Kikwete ambaye aliingia Ikulu mwaka 2010 kwa ushindi wa zaidi ya
asilimia 80. .
“Kwanza naomba niwashukuru wafanyakazi wote kwa
kukutana tena Mwanza. Wakati naanza urais mwaka 2006 sherehe zangu za
kwanza za Mei Mosi zilifanyika Mwanza, na furaha kubwa sherehe za mwisho
tena nafanyia Mwanza. Katika kipindi changu cha uongozi nimefanya mambo
mengi kushugulikia changamoto za wafanyakazi.”
Bango la walimu lamkuna JK..
Rais pia hakusita kueleza jinsi alivyokunwa na
ujumbe uliokuwa umeandikwa kwenye mabango ya vikundi kadhaa vilivyopita
mbele yake mwanzoni mwa sherehe hizo, hasa bango la walimu lililokuwa na
ujumbe usemao “shemeji unatuachaje”.
No comments:
Post a Comment