Maafisa nchini Pakstan wanasema kuwa
watu 43 wameuawa katika shambulizi lliliofanywa ndani ya basi
lililokuwa limewabeba waislamu wa asili ya kishia katika mji mkubwa wa
Karachi.
Polisi wanashuku kuwa shambuliz hilo limetekelezwa na kundi la wasuni wenye msimamo mkali.
Basi hilo lilikuwa limewabeba watu sitini kutoka katika jamii ya waislamu wa kishia walio wachache nchini Pakistan.
Maafisa wanasema kuwa watu sita waliokuwa na bunduki kwenye pikipiki walilazimisha basi hilo kusimama.
Waliingia katika basi hilo na kuanza kufyatua risasi kiholela.
Wengi waliouawa ni wanawake na watoto.
Baada ya mashambulizi hayo washambuliaji hao wanasemekana kutoweka kwa urahisi.
Mkuu wa polisi mkoani humo Ghulam Haider Jamali amesma huenda shambulizi hilo lilifanywa na kundi linaloshikilia itikadi kali lililokuwa limepigwa marufuku.
Hivi majuzi lilihusika vile vile kuwapiga risasi maafisa wakuu wa polisi huko Karachi.
Picha za video za shambulizi hilo zinaonesha basi lililo na mashimo mengi likivuja damu.
Makundi ya Taliban na makundi mengine ya wa-Sunni yamelaumiwa kwa kuwalenga wa-Shia nchini Pakistan.
Takwimu zinaonesha kuwa Pakistan inaasilimia 20% ya waislamu wa dhehebu la washia na asilimia 70% ya waSunni.
Dhehebu la WaIsmaili Shia, wanatofautiana na waislmu wengine kwa kumuamini Ali ,mkaza mwanawe mtume Mohammed.
No comments:
Post a Comment