Kiinua mgongo cha wabunge kimeongezeka?
(Makala ya Februari 2014)
Mnamo siku ya Alhamis tarehe 30 Januari, 2014 gazeti la kila siku la lugha ya kimombo The Citizen liliandika habari kuwa kiinua mgongo cha wabunge mwaka 2015 itakuwa shilingi milioni 160 sawa na nyongeza ya asilimia 274 kutoka walichopokea mwaka 2010. Habari hiyo imezua mjadala kwenye mitandao ya kijamii ambapo baadhi ya wabunge wamebishana kuhusu ukweli wa habari hiyo. Kwa vyovyote vile wabunge wote bila kujali itikadi za vyama vyao wataungana mkono katika jambo hili kama lile la posho. Naibu Spika wa Bunge amenukuliwa na vyombo vya habari akisema habari hii sio ya kweli. Vile vile tayari baadhi ya wafuasi wa wabunge wa chama kikuu cha upinzani nchini wameanza kufanya kampeni kuwa habari hii sio ya kweli. Wabunge wa vyama vyote vikuu nchini wanakanusha. Wameungana kwenye maslahi yao. Ukweli ni upi?
Kabla ya kuthibitisha kama Kiinua mgongo cha wabunge kimeongezeka au la ni vema kufahamu msingi wa kisheria wa kiinua mgongo ambacho sasa wananchi wamebatiza jina jipya la Kiinua Mdomo! Sheria ya Mafao ya kustaafu ya Wanasiasa (The political Service Retirement Benefits Act of 1999) kifungu cha 21 inaweka misingi ya kisheria ya malipo ya kiinua mgongo kwa wabunge. Kifungu cha 21(1) kinasema “Kiongozi aliyeshika nafasi ya Ubunge, mara baada ya kukoma kushika nafasi hiyo, atalipwa kiinua mgongo sawa na asilimia arobaini ya mshahara wake wa kila mwezi na atalipwa kwa mkupuo”. Kifungu cha 21(2) “Malipo yatakokotolewa kwa msingi wa idadi ya miezi ambayo mbunge ameshika nafasi hiyo na 21(3) kinasema Mbunge aliyemaliza muda wake atalipwa posho ya kumaliza muda (winding up allowance) sawa na asilimia ishirini ya jumla ya mishahara aliyopokea ya miezi ishirini na nne. Huu ndio msingi wa kisheria.
Nini kilitokea Bunge la Nane?
Wabunge waliomaliza muda wao mwaka 2005 walilipwa jumla ya shilingi milioni ishirini kama kiinua mgongo kwa kutekeleza sheria tajwa hapo juu kikamilifu.
Nini kilitokea Bunge la Tisa?
Wabunge waliomaliza muda wao katika Bunge la Tisa walilipwa jumla ya shilingi milioni 72. Sheria ilifuatwa kwa kifungu cha 21(1) ambapo kila Mbunge alilipwa kwanza asilimia 40 ya mishahara ya miaka mitano. Baada ya hapo sheria ikawekwa pembeni. Kila Mbunge alilipwa asilimia nyingine 60 ya kiinua mgongo kama ‘winding up allowance’ na pia asilimia 40 ya kiinua mgongo kama posho ya usumbufu (disturbance allowance). Kwa hiyo kimsingi mwaka 2010 kiinua mgongo cha Wabunge kililipwa mara mbili ya kiwango kilichopaswa kulipwa kisheria. Mapendekezo ya malipo haya yalitolewa na Tume ya Bunge na kuidhinishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kiinua Mdomo kitaongezeka mwaka 2015?
Ni dhahiri Wabunge watalipwa zaidi mwaka 2015 kwa sababu mishahara yao imeongezeka maradufu. Kwa kuwa Mshahara wa wabunge kwa Mwezi sasa ni shilingi milioni 3.4 (Mapato yote ya Mbunge kwa mwezi ni shilingi 11.2m bila kuweka posho za vikao (136m kwa mwaka) na posho za kujikimu (121m kwa mwaka)), na kwa kuwa kanuni ya kukokotoa kiinua mdomo sasa itakuwa ni ile ya mwaka 2010, basi kila Mbunge atapata jumla ya shilingi 163.2 milioni. Kwa hiyo kiinua mdomo cha waheshimiwa wabunge kimeongezeka.
Ongezeko la kiinua mdomo sio la kisheria. Iwapo wabunge wangetekeleza sheria ya mafao wangepaswa kulipwa shilingi milioni 97.9 tu. Hizi ni sawa na asilimia 40 ya mishahara ya miezi 60 jumlisha asilimia 20 ya mishahara ya miezi 24.
Kiufupi tunaweza kusema Dola imeamua kuwahonga wabunge kwa malipo haya. Wananchi wakienda mahakamani kutaka tafsiri ya kisheria, mahakama inaweza kupunguza malipo haya na kuhakikisha ni malipo ya kisheria tu ndio yanalipwa. Tunataraji wabunge wazalendo watatoka wazi na kukataa nyongeza yeyote ya kiinua mdomo ambayo ni kinyume cha sheria. Sasa wajitokeze.

No comments:
Post a Comment