Meya wa jimbo la Baltimore nchini Marekani Stephanie Rawlings-Blake.
Meya wa Mji wa Baltimore nchini Marekani, Stephanie Rawlings-Blake,
amesema kuwa amehudhunishwa na kuvunjwa moyo baada ya polisi sita
kushtakiwa, kufuatia kifo cha mwananaume mweusi, Freddie Gray.Polisi
mmoja anakabiliwa na mashtaka ya mauaji huku wengine watano wakikabiliwa
na mashtaka ya kuua bila kukusudia.
Maandamano yaliyofanywa katika jimbo hilo.
Tangazo hilo lilisababisha watu kusherehekea kwenye mji wa Baltimore
lakini wengine waliiendelea kuandamana.Wakili anayewakilisha chama cha
polisi katika mji huo, alilaani kile alichokitaja kuwa kuharakisha
katika kuwafungulia mashtaka polisi hao.
Rais wa Marekani Barack Obama anasema kuwa, ni muhimu uchunguzi wa
kina ukafanyika ili kubainisha ukweli kuhusu kile kilichosababisha kifo
cha bwana Gray.
No comments:
Post a Comment