Polisi mjini Songea, imezuia mkutano wa Chama cha Wananchi (CUF) uliokuwa ufanyike kwenye Viwanja vya mikutano vilivyopo eneo la Majengo Manispaa ya Songea.
Mkutano huo ambao Naibu Katibu Mkuu Bara wa chama
hicho, Magdalena Sakaya alitarajiwa kuwahutubia mamia ya wakazi wa
manispaa hiyo wakiwemo makada wa chama chake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela
alipopigiwa simu na mwandishi wa gazeti hili kwa lengo la kutaka
ufafanuzi alisema kuwa hana taarifa zozote na alipomuuliza mkuu wa
Polisi wa Wilaya ya Songea(OCD) naye alikataa kuwa hana barua ya aina
yoyote ya CUF ya kuomba kufanya mkutano na amewataka wafuate taratibu
zinazotakiwa na wakitaka kuanzia kesho wafanye mkuatano hata kwa siku
kumi.
Baadhi ya Waandishi wa habari ambao walifika
kwenye eneo la tukio akiwemo mwandishi wa gazeti hili kwenye viwanja
hivyo vya mikutano na kukuta hali ya sintofahamu baada ya baadhi ya
makundi ya watu yakiendelea kulalamika kuzuiliwa kufanyika kwa mkutano
huo ambao baadhi ya viongozi wa chama hicho waliwaeleza waandishi wa
habari kuwa mkutano huo ulikuwa na lengo la kusaidia kuhamasisha
wananchi wajitokeze kwa wingi katika kujiandikisha kwenye daftari la
kudumu la kupiga kura na si vinginevyo.
Katibu wa chama hicho wa Wilaya ya Songea Khamis
Khais alipohojiwa na waandishi wa habari alisema kuwa tangu Aprili 29
mwaka huu chama chake kiliandika barua ya kuomba kibali cha kufanya
mkutano wa nje kwenye viwanja vya majengo kwa jeshi la polisi kituo
kikuu cha Songea ambapo barua hiyo ilipokelewa na kusainiwa kwenye
kitabu chao cha CUF (dispachi ) na kujibiwa kwa mdomo kuwa wakaendelee
kufanya mkutano huo jambo ambalo CUF imetekeleza kwa kuwahamasihsa
wananchi wahudhurie kwa wingi kwenye mkutano ambao umezuiliwa hata kabla
ya kuanza licha ya wananchi wameshafika kwenye viwanja hivyo.
No comments:
Post a Comment