Polisi
wa Ujerumani wamefuta mashindano ya kimataifa ya kuendesha baiskeli
yaliyotarajiwa kufanyika ijumaa katika mji wa Frankfurt, kwa hofu ya
shambulio la kigaidi.
Polisi wanashuku kwamba wawili hao walikua na mpango, wa kufanya mashambulizi wakati wa mashindano ya kuendesha baiskeli ambayo yamevutia wachezaji wengi duniani.
Mwanamume na mwanamke wa miaka 30 walikua wakifuatwa na majasusi kwa majuma mawili baada ya kutumia majina bandia wakati wakinunua kemikali inayoweza kutengeneza mabomu.
Polisi waliamua kuvamia makaazi yao baada ya mwanamume mmoja anayeaminika kuwa na uhisiano na makundi ya kisiilamu yenye misimamo mikali kuonekana nje ya nyumba yao mara kadhaa.
Polisi walipata mabomba ya kutega mabomu, silaha na kemikali.
Haijabainika iwap wawili hao walikua wakishirikiana na mtandao fulani.
No comments:
Post a Comment