USALITI? Huenda maumivu ya mapenzi yakazidi kumuandama msanii wa
muziki Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ baada ya gazeti hili
kunasa picha za mchumba’ke Shamsa Ford akiwa katika mahaba mazito na
msanii mwanaume mwingine aliyedaiwa kuwa ni mchepuko wake, Rammy Galis,
Amani lilifuatilia hatua kwa hatua.
Staa wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford akipozi kimahaba na Rammy Galis.
Ishu hiyo ‘ilidakwa’ na ‘balozi’ wa gazeti hili usiku wa Jumapili
iliyopita ndani ya Ukumbi wa New Maisha, Masaki jijini Dar kulipokuwa na
onesho la Mrs. Mabeste Charity hafla iliyokusanya mastaa kibao na
watoto wengi wa mjini.
Katika pitapita zake huku akikodoa macho kila
kona ndani ya ukumbi huo, mwandishi wetu alibahatika kuwaona wawili hao
wakiwa wamegandana kwa staili ambayo si ya kujadili katiba mpya huku
ukaribu na kutazamana kwao kukiwa na maswali mengi kuliko majibu.
...Wakisakata rumba.
Hata hivyo, umbali wa mkao wao ulianza kupungua kila dakika moja
ilipopita wakawa wanabadili mapozi yakiwemo kutazamana kimahaba na
kushikana kwa kujitawala.
Baada ya kuhakikisha kuwa amepata picha za ushahidi wa kutosha,
mwandishi wetu aliwafuata wawili hao na kumuuliza Shamsa kama huyo ndiye
mbadala wa Nay, akamwambia mwandishi kuwa haikuwa kazi yake kujua kwani
pale walikuwa eneo la starehe hivyo hawakutaka bughudha na karaha
yoyote.
Staa wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford.
“Ebwana ee, mbona hivyo jamani? Siyo kazi yako kujua huyu ni nani
kwangu, ni msanii mwenzangu na hapa tuko kwenye sherehe na hatuhitaji
usumbufu wowote,” alisema kwa mkato Shamsa.
Kwa upande wake Galis, alisema hana cha kusema kwani hakuwa eneo la mahojiano.
“Kaka huyu ni msanii mwenzangu na hapa si sehemu ya mahojiano,” alijibu.
Nay alipopigiwa simu alisema: “Hawa wanawake wa Bongo Muvi utawaweza! Ila nitadili naye.”
No comments:
Post a Comment