Viongozi wa upinzani nchini DRC wameeleza kwamba wako tayari kwa
mazungumzo na Rais Joseph Kabila kabla ya kufanyika uchaguzi, wakiserma
jambo hilo huwenda likasaidia kuepuka migogoro wakati wa uchaguzi.
Matamshi hayo yametolewa kufuatia ripoti kwamba Rais Kabila yuko
tayari kuzungumza na upinzani juu ya matayarisho ya uchaguzi mkuu nchini
humo.
Mwakilishi wa chama cha UDPS Ribes Mikindo, alithibitisha kuwepo na
ripoti hiyo alipozungumza na VOA, akieleza kwamba jambo kubwa litakuwa
kuona ni jinsi gani uchaguzi wa nchi utaweza kufanyika ikiwa ni pamoja
na uchaguzi wa wabunge .
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Kambale Mota huko mashariki ya mwa
Congo amesema mawasiliano kati viongozi wan chi hiyo ni jambo jema
lakini pia inaweza kuwa shida ikiwa watakwenda kinyume cha katiba na
maslahi ya wakazi wa Congo.
Uchaguzi mkuu wa Congo unatazamiwa kufanyika baadae mwaka 2016, na
upinzani unapinga kwa Rais Kabila kugombania mhula mwengine kwani
inakwenda kinyume na katiba ya nchi.
No comments:
Post a Comment