Saturday, 2 May 2015

Wafilipino kumshangilia Pacquiao......

                        
Wakati huohuo wito umetolewa kwa wakazi wa kisiwa kimoja cha Philippines kwamba watumie umeme kwa kiasi kidogo ili kumwangalia katika runinga zao hapo Jumapili shujaa wao Mfilipino mwenzao , Manny Pacquiao (36) atakapokuwa akipambana na Mmarekani Floyd Mayweather (38) kwenye ulingo wa shindano la ndondi linalotajwa kuwa kubwa zaidi siku za hivi karibuni.
Wakazi hao wameshauriwa na kampuni ya umeme nchini humo Palawan kuzima vifaa vinavyotumia umeme majumbani kama friji, mashine za kufua nguo na pasi ili kuhifadhi umeme kwa ajili ya  kuwashia runinga zao.

Manny Pacquiao akipima uzito.

Ushauri huo umetolewa kwani kisiwa hicho hukumbwa na upungufu wa umeme mara kwa mara, hivyo ni sharti wafuate maagizo hayo ili wasikose kushuhudia na kumshangilia kinara wao huyo atakayeshiriki pambano hilo litakalofanyika huko Las Vegas Jumamosi usiku saa za Marekani.

Ndilo pambano lililovutia fedha zaidi kuwahi kutokea.

No comments:

Post a Comment