Thursday, 30 April 2015
In the village of Bulati, Ngorongoro recently/ Nikiwa katika kijiji cha Bulati Ngorongoro hivi karibuni, Dr. ELIAMANI LALTAIKA a friend and a realy good man .. HE believes in his community for years and years .. kijana toka familia MASIKINI KABISA alisomeshwa na wazungu walipata kuwa rafiki zangu pia .. na sasa anarudisha kwenye jamii yake alichobarikiwa na MUNGU ili pawepo na usawa .
WAISLAM WACHARUKA ... WAIPA SEREKALI 15 DEYZ .. >>
Jumuiya na Taasisi za Kiisalam nchini, imetoa tamko na kuipa serikali siku 15 kabla ya kufanya maandamano nchi nzima kuelekea Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakidai kufunguliwa kwa madrasa zilizofungiwa kwa kuhusishwa na kutoa mafunzo ya ugaidi.
Masharti mengine ni kuachiliwa huru au kwa dhamana masheikh na maimamu waliokamatwa wakituhumiwa kutoa mafunzo na mazoezi ya kigaidi.
Maeneo ambayo madrasa hizo zaidi ya 10 zimefungwa ni katika mikoa ya Kilimajaro, Dodoma na Mtwara. Tamko hilo pia lilisema jeshi hilo linawatuhumu kwa kukusanya watoto na kuwafundisha elimu ya dini katika mazingira yasiyofaa na kuwapo kwa taarifa za watu wenye milipuko misikitini na kujihusisha na ugaidi.
Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Sheikh Musa Kundecha, alisema jeshi hilo limekuwa likiwakamata watu hao usiku na kuwapeleka katika vituo vya polisi, na kuwahoji.
Alisema jeshi hilo limekuwa likifanya kazi za maofisa wa ustawi wa jamii na elimu, kufanya ukaguzi katika maeneo ambayo watoto hao wanafundushwa elimu ya dini ya kiislamu.
“Mkakati wa operesheni hii unakiuka utu, haki za binadamu, kikatiba na ni uchochezi dhidi ya Waislamu kuwafanya wachukiwe na jamii, tunawatunza yatima katika maeneo jirani na madrasa na kuwapa elimu ya kidini siyo kosa, tunatimiza wajibu wa kidini. Wajibu wa serikali ni kutulinda, lakini tunawekwa katika mazingira ya hatari,” alisema Kundecha.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga, alisema ulifanikiwa utafiti, kabla ya jeshi hilo kuchukua hatua za kufunga baadhi ya madrasa na kuwakamata watu hao.
“Katika maeneo ya mikoa hiyo ni kweli kuna suala hilo, na watoto ambao wana umri wa kuwa shule walikutwa pale, hivyo tukataka kufahamu na yajulikane mafunzo wanayopewa,” alisema Nantanga.
Alisema kuendelea kushikiliwa kwa baadhi ya watu waliokamatwa na kunyimwa dhamana kunatokana na jeshi hilo kutojiridhisha au kutokamilika kwa taratibu za dhamana.
“Pale mtuhumiwa atakapoachiwa, ni lazima polisi wajiridhishe kabla ya kumpatia dhamana mtuhumiwa. Hadi hivi sasa, kama wizara hatujapokea tamko lolote kuhusu jambo hili, tunasubiri kupokea rasmi tamko, na tutaliweka mezani na kulifanyia kazi,” aliongeza.
CHA WENE AWAKATAA SELCOM WAZIWAZI , AWATAKA WAPISHE WENGINE WENYE UWEZO !...
Waziri wa Nishati G. Simbachawene aiagiza TANESCO kuvunja mkataba na Selcom kuuza umeme wa Luku baada ya kushindwa kazi...leo ni siku ya tatu wateja wa Tanesco hatuwezi kununua Luku Kwa Kutumia Mitandao ya Simu, Hili limekuwa Tatizo sugu linalojitokeza mara kwa mara
Selcom ni Platform inayotumiaka na Tanesco kuunganisha kati ya mitandao ya Simu na Mitambo ya Tanesco..
Baada ya Taarifu hiyo Lemutuz aliandika hivi:
- Saafi sana tunataka Viongozi wanaoweza kutoa majibu magumu kwa matatizo magumu, Waziri hawezi kukurupuka kuna wasaidizi wake maalum wengi wa kumfanyia utafiti kabla ya kutoa maamuzi mazito kama haya tena kwa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi, Wahusika wote wa Luku walishafika mahali wakajisahau na kudhani kwamba na wao ni Serikali flani ndani ya Serikali yetu.
udk blog..
WEMA KAOLEWA ...: ... AISEE !
Staa wa filamu za Kibongo,Wema Sepetu amekiri kufunga ndoa bomani hivi karibuni ambayo ilihudhuliwa na watu wachache. Akizungumza na Clouds FM alisema kuwa aliamua kufunga ndoa ya siri kwa kuogopa kupigwa 'juju' na mumewe angeshindwa kumuoa.
‘’Mume wangu ni Mtanzania na siyo maarufu na ndoa yangu ilihudhuriwa na ndugu zangu wachache na ndugu wa mume wangu sikutaka watu wengi niliogopa kupigwa juju na mume wangu asingenioa,’’alisema Wema.
Hata hivyo alipoulizwa kuhusu tatizo lake la kutoshika mimba alisema kuwa mumewe amelikubali na hana tatizo
Hongera sana Wema.
MAANDAMANO MAPYA MAREKANI ....>>>
Kumetokea maandamano mapya nchini
Marekani katika mji wa Baltimore kufuatia kifo cha kijana mweusi Freddie
Gray aliyekufa kutokana na majeraha akiwa mikononi mwa polisi. Mamia ya
watu wameandamana katika mitaa, wakionyesha ujasiri licha ya hali mbaya
ya hewa iliyokuwepo.
Mtetezi wa haki za binadamu, Mchungaji Al Sharpton, ameitisha mkutano mjini Baltimore ili kuimarisha uhusiano baina ya polisi na wanajamii.
KI MOON ASIKITISHWA NA MAPIGANO YEMEN ...>
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban
Ki-moon ameelezea tahadhari yake kuhusiana na hatari ya raia kuendelea
kupigana, Nchini Yemen.
Mashambulizi katika majumba ya raia zikiwemo hosptali na maghala ya vifaa vya misaa ya kibinadamu yamekuwa yakiendelea.
Kumekuwa na taarifa watu wenye silaha wamekuwa wakiwateka raia katika mitaa ya Aden.
Shirika la Umoja wa mataifa la misaada ya chakula limesema halina jinsi zaidi ya kusitisha mipango yake ya kusambaza misaada kutoka na tatizo la mafuta.
Kwa sasa mapigano makali yanaendelea katika mipaka ya eneo la Yemen na Saudia Arabia.
ISIS NI NOOOMA ! ! ,,,>> MAUAJI YA KUTISHA HUKO SYRIA NA IRAQ
Mpiganaji wa ISIS akinyanyua tofali la zege kumpiga mmoja wa wanaume waliokamatwa kwa kuua wanawake.
WAPIGANAJI wa ISIS wamefanya mauaji ya kutisha kwa mateka wawili wa
kiume waliotuhumiwa kuwaua kwa kuwapiga virungu wanawake watatu huko
nchini Iraq.ISIS waliwapiga watuhumiwa hao kwa matofali ya zege kichwani hadi kufa ikiwa ni adhabu kwa kitendo chao cha kuiba na kuwaua wanawake watatu. Tukio hilo limefanyika katika Mkoa wa Nineveh huko kaskazini mwa Iraq.
Katika tukio lingine lililowekwa katika mitandao ya kijamii wiki hii linaonyesha picha za wanaume wawili wengine wakichinjwa na kundi hilo la ISIS katika Kijiji cha Jarnyah, Magharibi mwa Raqqa nchini Syria.
Wanaume hao wanadaiwa kuuawa baada ya kukamatwa wakijihusisha na vitendo vya kishirikina.
Wanaume hao waliokuwa wamefungwa vitambaa usoni wanaonekana wakiwa wameweka vichwa vyao juu ya magogo huku mapanga yakiwa kwenye shingo zao na wananchi wakishuhudia tukio hilo.
Wiki iliyopita, picha za wapiganaji hao wa ISIS wakiwapiga mawe hadi kufa mashoga wawili huko Syria nazo zilionekana kwenye mitandao ya kijamii.
Kabla ya kuwaua mashoga hao, ISIS waliachia picha zilizokuwa zikiwaonyesha mashoga hao wakiwa wamekumbatiana na kuwaambia kuwa wamewasamehe dhambi zao kabla ya kuwapiga kwa mawe hadi kufa.
MGM GRAND ... KUELEKEA MPAMBANO WA KIHISTORIA KATI YA MONEY NA PACMAN
Floyd Mayweather (kushoto) na Manny Pacquiao wakipozi na mkanda wa WBC jana wakati wa mkutano na wanahabari.
SIKU mbili tu zimebaki kuelekea mpambano wa kihistoria wa ngumi za
kulipwa utakaowakutanisha mabondia Floyd Mayweather (Money) na Manny
Pacquiao (Pacman) ndani ya Ukumbi wa MGM Grand jijini Las Vegas,
Marekani.Mpambano huo umekuwa gumzo kote duniani kwa sababu wapinzani hao wamekuwa wakitafutana kwa muda mrefu kabla ya kukubali kupanda ulingoni na kuzichapa Mei 2 mwaka huu ambapo kwa muda wa huku itakuwa alfajiri ya Mei 3.
Money na Pacman watakomba kiasi cha dola za Kimarekani milioni 300 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 589 za Kitanzania na iwapo Mayweather atashinda pambano hilo ataweka kibindoni dola za Kimarekani milioni 180 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 353 za Kitanzania ambayo ni asilimia 60 ya kiasi cha fedha kinachoshindaniwa.
ZIFUATAZO NI BAADHI YA DONDOO ZA MPAMBANO HUO:
MIKWANJA
$300 milioni - Kiasi cha mkwanja uliotengwa kwa ajili ya pambano hilo ambapo asilimia 60 itakwenda kwa Mayweather huku asilimia 40 ikikombwa na Pacquiao (Pacman)
$321.43 - Kiasi alichotumia Mayweather kwa upande wa vyakula wiki kadhaa akijiandaa kwa pambano hilo.
$2 - Kiasi cha fedha alizokuwa akilipwa Pacquiao kwa kila pambano wakati wa ukuaji wake huko Ufilipino
$250,000 - Kiasi kilichowekwa kubashiri mpambano huo kati ya mwanamuziki Diddy na Mark Wahlberg
$600 milioni - Jumla ya kiasi cha fedha atakachokuwa ametengeneza Mayweather kutokana na ubondia baada ya pambano lake na Pacquiao
$150 - Gharama za kuangalia pambano hilo kupitia televisheni zitakazokuwa zimefungwa katika hoteli ya MGM
£19.95 - Gharama za kuangalia pambano hilo kupitia Kituo cha Sky Sports huko Uingereza
$99.95 - Gharama ambazo watalipa mashabiki waliopo Amerika kuangalia pambano hilo kupitia HBO au Showtime
$74 milioni - Mapato yanayotarajiwa kupatikana kutokana na tiketi zilizopangiwa kiwango kati ya $1,500 na $10,000
$5.6 milioni - Kiasi kilicholipwa na Tecate kudhamini pambano hilo.
$10,000 - Malipo atakayolipwa refa wa mpambano huo, Kenny Bayless
WAPIGANAJI
47 - Idadi ya mapambano ya kimataifa na ushindi ambao ameupata bondia Mayweather
55.3% - Asilimia za ushindi wa Mayweather kwa knockout (KO)
62 - Idadi ya mapambano ya kimataifa aliyopigana Pacquiao
66.6% - Asilimia za ushindi wa Pacquiao kwa knockout (KO)
39 - Wastani wa makonde aliyotupa Mayweather kwa kila raundi tangu alipoanza mapambano ya kimataifa.
66 - Wastani wa makonde aliyotupa Pacquiao kwa kila raundi tangu alipoanza mapambano ya kimataifa.
74 - Jumla ya umri wa mabondia hao (Mayweather ana umri wa miaka 38 huku Pacquiao akiwa na miaka 36)
Milioni 5.8 - Idadi ya wafuasi wa Mayweather katika mtandao wa Kijamii wa Twitter; Pacquiao ana wafuasi milioni 1.8
309 - Idadi ya maili ambazo Pacquiao alisafiri kwa basi lake la kifahari kutoka Los Angeles kwenda Las Vegas kwa ajili ya mpambano huo.
Manny akiwa kwenye basi lake la kifahari wakati akielekea Las Vegas akitokea Los Angeles alipokuwa ameweka kambi.
MPAMBANO36 - Idadi ya dakika ambazo kila bondia atatumia kwenye ulingo iwapo pambano litachukua muda wote uliopangwa.
5 - Idadi ya miaka tangu pambano hili la kihistoria lianze kujadiliwa kwa undani.
UKUMBI
16,500 - Idadi ya viti vya wageni wanaoruhisiwa kuingia katika Ukumbi wa MGM Grand wakati wa pambano hilo
9,000 - Idadi ya watu walioajiriwa katika Ukumbi wa MGM Grand
100,000 - Idadi ya watu wanaotarajiwa kuwepo katika hoteli ya MGM Grand kati ya Ijumaa na Jumamosi
7,000 - Idadi ya vyumba vilivyopo katika hoteli ya MGM Grand
VYOMBO VYA USALAMA VILIZEMBEA ,,,>> (GARISSA )
Waziri wa usalama wa ndani nchini
Kenya Generali Joseph Nkaiserry amekiri kwamba vyanzo na duru za
kijasusi zilitahadharisha lakini zilipuuzwa kabla ya shambulizi la Al
Shabaab katika chuo kikuu cha Garrissa.
Waziri Nkaissery ameongeza kusema shughuli za wokozi zilizofuata pia zilifanywa kiholela.
Baadhi ya Maafisa wakuu wa polisi wamesimamishwa kazi kufuatia shambulia hilo la Chuo Kikuu cha Garrissa.
WATOTO WAFANYA MBAYA BABA NA MAMA ,,,>>
POLISI katika Jimbo la Enugu, Nigeria, wanachunguza vifo ambapo wanaume wawili wasiokuwa ndugu, waliwaua baba na mama zao katika matukio mawili tofauti.
Mauaji hayo yalitokea Aprili 26 Jumapili iliyopita na Aprili 27 Jumatatu ya wiki hii sehemu tofauti ambapo muuaji wa kwanza, Chijioke Onyeke, alimkata baba yake kwa panga mnamo saa 12 jioni katika ugomvi usiofahamika chanzo chake katika kijiji cha Umuogboagu kaskazini mwa nchi hiyo.
Mtu huyo alifia katika hospitali ya St. Mary, kutokana na majereha ambapo mtuhumiwa alikamatwa.
Katika tukio jingine, Chidi Agbo, kutoka kijiji cha Igboeze, kaskasini mwa nchi hiyo, alimpiga mama yake hadi kumwua ambapo pia sababu ya kufanya hivyo haijulikani.
Chidi naye yuko mikononi mwa polisi.
source .. MTANDAO WA PULSE
MAYWEATHER HAKULITAKA PAMBANO NA PACQUIAO ,,,, >>
Kocha wa bondia Manny Pacquiao ,Freddie Roach ana wasiwasi huenda bondia Floyd Mayweather asitokeea kwenye mpambano wa mei 2.
"Sijui kwanini amekua mkimya sana kwenye mpambano huu maneno yake yana woga”
Hata hivyo Mayweather hakushangazwa na kauli hizo za kocha huyo na kudai "nitakuepo niliongea uchafu siku za nyuma lakini hili pambano linajiuza lenyewe”.
Pambano hili limeteka hisia kwa washabiki wa masubwi duniani kote huku homa ya mchezo ikiwa inapanda kila muda unavyozidi kukaribia pambano hilo hapo Mei 2.
PEARSON ATUKANA MWANDISHI ...>>
Meneja wa Leicester City, Nigel Pearson amemshambulia kwa matusi Mwandishi wa habari akimfananisha na ndege aina ya mbuni.
Bosi huyo wa Leicester alimtukana mwandishi Ian Baker aliyemuuliza swali kuhusu madhaifu ya wachezaji wake yaliyosababisha timu kuboronga msimu mzima.
Pearson, hakufurahishwa na namna alivyoulizwa na kuamua kumtukana mwandishi akisema: “Wewe lazima ni punguani sana, sana”.
TETESI ZA USAJILI ,,, >>
PSG wamvalia njuga Di Maria
*Arsenal, Man United vikumbo
matajiri wa Ufaransa, Paris St-Germain (PSG) wapo tayari kutoa pauni milioni 45 kumsajili winga wa Manchester United, Angel Di Maria.
Raia huyu wa Argentina aliyesajiliwa kiangazi kilichopita kutoka Real Madrid ameshindwa kuchanua kwenye Ligi Kuu ya England (EPL) na sasa PSG wanadhani watampa raha.
Di Maria (27) aliwagharimu United pauni milioni 59.7, akivunja rekodi ya usajili nchini Uingereza lakini Kocha Louis van Gaal amemchezesha namba tofauti bila mafanikio.
Katika mechi tano zilizopita alianzia benchi hivyo kuonekana kushindwa kutimiza kilichotarajiwa kutoka kwake, huku familia ikiwa haina raha baada ya wezi kujaribu kuvamia nyumba yake familia ikiwa ndani jijini Manchester.
Wezi hao walikimbia baada ya Di Maria kubonyeza kitufe cha kuita polisi na king’ora kulia nje ya kasri hilo. Amehamishiwa hotelini tangu wakati huo.
Hata hivyo, Man U wanadai hawana nia ya kumuuza winga huyu lakini PSG wanadaiwa watawajaribu kwa kuwasilisha ofa rasmi karibuni baada ya kushindwa kumsajili msimu uliopita.
United wanadaiwa kutia nia ya kumsajili mlinzi wa kati wa Athletic Bilbao, Aymeric Laporte, ambaye mkataba wake unasema anaweza kuuzwa ikiwa klabu inayomtaka itatoa pauni milioni 30.
Hata hivyo Man U watakabiliana na upinzani kutoka kwa Arsenal ambao pia wanataka kumsajili Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 21.
United wataongeza nguvu kwa chipukizi huyu iwapo mipango yao ya kumsajili mlinzi mahiri wa Borussia Dortmund, Mats Hummels.
Klabu ya Marseille ya Ufaransa inataka kuwasiliana na Manchester City kwa ajili ya kumchukua kocha wao wa timu ya vijana, Patrick Vieira ili awe kocha nchini mwake kuanzia msimu ujao.
Hata hivyo, City wanamthamini sana Vieira na si rahisi kumwachia aondoke, ambapo pia amekuwa akifikiriwa kupewa kazi ya kocha Manuel Pellegrini iwapo bosi huyo atafutwa kazi.
Tottenham Hotspur wanajaribu kumsajili kiungo wa Southampton, Morgan Schneiderlin, 25. Inaelezwa kwamba Saints wanataka pauni milioni 20 huku Spurs wakiwa tayari kuwapa kiungo wao, Andros Townsend, 23, au Benjamin Stambouli, 24, na kiasi kidogo cha fedha.
Spurs na Arsenal wamekuwa wakimtaka Scheiderlin tangu msimu uliopita na haijulikani kati ya watani hao wa kaskazini mwa London yupi atafanikiwa safari hii, au iwapo wote watamkosa.
Arsenal, Chelsea Spurs wanapigana vikumbo kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Luton, Charlie Patino mwenye umri wa miaka 11 tu.
Bosi wa Chelsea, Jose Mourinho amebainisha kwamba mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich ndiye atakuwa na kauli ya mwisho juu ya hatima ya mshambuliaji wao, Didier Drogba, 37, ambaye mkataba wake wa mwaka mmoja unamalizika kiangazi hiki.
Newcastle wanataka kumsajili mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Vijana ya England, Patrick Bamford aliyefunga mabao 19 akiwa kwa mkopo Middlesbrough kutoka Chelsea.
Manchester United wanataka kumsajili kipa wa Spurs, Hugo Lloris, 28, ikiwa kipa wao, David De Gea, 24, atarudi nyumbani kwao Hispania kujiunga na Real Madrid.
Mshambuliaji wa Arsenal, Theo Walcott, 26, amedai kwamba Arsenal ndio timu bora Ulaya kwa 2015, ikiwa ni dalili kwamba hataondoka Emirates.
Mmiliki wa Napoli, Aurelio De Laurentiis amemtaka kocha wao, Rafael Benitez kuacha mipango ya kurudi England ili abaki na vijana wake.
Torino wanasema huenda wakamuuza beki wao, Matteo Darmian wakipata ofa ‘kichaa’. Arsenal na Manchester United ni kati ya klabu zinazohusishwa na mchezaji huyu wa kimataifa wa Italia.
Mshambuliaji wa Newcastle, Adam Campbell, 21, anafanya majaribio katika klabu ya West Bromwich Albion kwa minajili ya kusajiliwa huko.

WANAFUNZI WAPEWA TAHADHARI BURUNDI ,,,, >>
Wanafunzi katika chuo kikuu cha
Burundi mjini Bujumbura, wanasema kuwa serikali imewaagiza kufungasha
virago vyao na kuondoka chuoni hapo mara moja kwani chuo hicho
kinafungwa.
Watu watano wameripotiwa kufariki tangu kuzuka kwa ghasia hizo siku kadhaa zilizopita.
Umoja wa mataifa umeonya kuwa huenda taifa hilo likaingia katika lindi la mzozo wa kisiasa, iwapo ghasia hizo zitakithiri, mwezi mmoja tu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu hapo mwezi Juni.
Maafisa wakuu wa umoja wa mataifa na mwanadiplomasia wa Marekani, kwa sasa wanashauriana na serikali ya Burundi, ili kukabiliana na taharuki hiyo ya kisiasa.
Mapema polisi walitibua maandamano ya watu waliokuwa na lengo la kuweka vizuizi kwa raia Nkurunzinza kuwasilisha stakabadhi zake hii leo kama mgombea wa urais wa nchi hiyo.
WAGENI WALIOPO SA WARUDI MAKWAO '' MUGABE'' ...
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, jumatano aliwasihi wahamiaji
walioshambuliwa nchini Afrika kusini kurejea majumbani mwao. Matamshi
yake yalikuja mwishoni mwa mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika-SADC unaoangalia namna eneo hilo linavyoweza
kujiendesha kiviwanda.
Mwishoni mwa mkutano wa siku moja viongozi kutoka SADC walitoa tamko la pamoja walisema eneo hilo liliridhika na hatua ambayo serikali ya Afrika kusini imechukua kuhakikisha kwamba mashambulizi ya hivi karibuni juu ya wahamiaji hayatatokea tena.
Bwana Mugabe ambaye ni mwenyekiti wa SADC na Umoja wa Afrika aliwaambia waandishi wa habari kwamba hakukuwa na haja kwa wa-Afrika kwenda Afrika kusini, taifa la pili lenye uchumi mkubwa sana katika bara la Afrika. “Watu wetu hawana haja ya kukimbilia nchini Afrika kusini. Wanafikiri Afrika kusini ni peponi kwetu katika eneo la kusini mwa Afrika. Ndio, kuna maendeleo.
Zaidi. Lakini nenda huko na utaona kwamba wa-Afrika bado wapo chini. Ni wazungu ambao wanaishi maisha bora Zaidi”.
Makadirio yanaonesha kwamba wazimbabwe ndio kundi kubwa sana la wahamiaji walioathirika huko Afrika kusini kutokana na mashambulizi ya wageni. Wanakadiriwa kuwa watu milioni tatu.
Kabla ya kwenda kwenye mkutano huo mjini Harare, Rais wa Afrika kusini, Jacob Zuma alisema alitaka suala hili kujadiliwa japokuwa halikuwemo kwenye ajenda. Rais wa Malawi Peter Mutharika pia alieleza kwamba alitaka SADC kuzungumzia suala la mashambulizi ya wageni.
Rais wa Nigeria anayeondoka madarakani, Goodluck Jonathan alimuagiza
kaimu balozi wa Nigeria kwa Afrika kusini, kupinga namna Pretoria
ilivyoshughulikia mashambulizi ambayo yalidaiwa kusababisha vifo vya
watu saba.
Umoja wa Afrika-AU ulisema unakaribisha juhudi za Afrika kusini za kumaliza ghasia lakini kazi zaidi lazima ifanywe ili kuwalinda wa-Afrika na wahamiaji wengine wa kigeni.
Mwishoni mwa mkutano wa siku moja viongozi kutoka SADC walitoa tamko la pamoja walisema eneo hilo liliridhika na hatua ambayo serikali ya Afrika kusini imechukua kuhakikisha kwamba mashambulizi ya hivi karibuni juu ya wahamiaji hayatatokea tena.
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe
Bwana Mugabe ambaye ni mwenyekiti wa SADC na Umoja wa Afrika aliwaambia waandishi wa habari kwamba hakukuwa na haja kwa wa-Afrika kwenda Afrika kusini, taifa la pili lenye uchumi mkubwa sana katika bara la Afrika. “Watu wetu hawana haja ya kukimbilia nchini Afrika kusini. Wanafikiri Afrika kusini ni peponi kwetu katika eneo la kusini mwa Afrika. Ndio, kuna maendeleo.
Zaidi. Lakini nenda huko na utaona kwamba wa-Afrika bado wapo chini. Ni wazungu ambao wanaishi maisha bora Zaidi”.
Makadirio yanaonesha kwamba wazimbabwe ndio kundi kubwa sana la wahamiaji walioathirika huko Afrika kusini kutokana na mashambulizi ya wageni. Wanakadiriwa kuwa watu milioni tatu.
Kabla ya kwenda kwenye mkutano huo mjini Harare, Rais wa Afrika kusini, Jacob Zuma alisema alitaka suala hili kujadiliwa japokuwa halikuwemo kwenye ajenda. Rais wa Malawi Peter Mutharika pia alieleza kwamba alitaka SADC kuzungumzia suala la mashambulizi ya wageni.
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan
Umoja wa Afrika-AU ulisema unakaribisha juhudi za Afrika kusini za kumaliza ghasia lakini kazi zaidi lazima ifanywe ili kuwalinda wa-Afrika na wahamiaji wengine wa kigeni.
Wednesday, 29 April 2015
AJIRA NI ZAIDI YA HIROSHIMA aka NYUKLIA BOMB .
KILICHOTOKEA BALTMORE na SA, ni kaka na dada tatizo la ajira .. population ya watu weusi kule BALTMORE ni kwa asalimia 63-75% kati ya hao % 11-35 hawana kazi (AJIRA) ...
Na South Africa napo waliotajwa kuongoza vurugu ni JOBLESS wasio na kazi wanaoishi mabwenini...
Vurugu za BALTMORE si kwa sabau ya GRAY tu ! Na SA pia .
Marekani : HASARA ILIYOPATIKANA BALTMORE ni dolla milioni 79.
Tanzania tujifunze na tusipiuze wenzetu wakinyolewa ... Zetu tutie ...
Tutokevipi?

Tuesday, 28 April 2015
Liverpool yachapwa na Hull City 1 - 0
Liverpool
imezidi kujiweka katika hali ngumu ya kuingia katika nne bora ya ligi
hiyo baada ya kukubali kichapo cha bao moja kwa bila kutoka kwa Hull
City.
Ligi hiyo itaendelea tena leo hii kwa mchezo mmoja kupigwa wakati Chelsea itakapokuwa ugenini kukipiga dhidi ya Leicester City.
JESHI LA NIJERIA LAWAOKOA WASICHANA 293 WALIOTEKWA NA BOKO HARAAM ...!!
Jeshi la Nigeria limesema limewaokoa
watoto wa kike mia mbili na tisini na tatu kutoka katika kambi ya Boko
Haram iliyoko katika msitu wa Sambisa, kaskazini mashariki mwa nchi
hiyo. Jeshi hilo limesema watoto hao waliokolewa si kati ya wale
waliotekwa mwaka mmoja uliopita na kundi la kiislamu katika eneo la
Chibok.
"ni muda mfupi tu uliopita, wanajeshi wetu wameingia katika msitu wa Sambisa, kutokea upande wa Alafa, ambapo walikuta kambi nne zinazomilikiwa na wapiganaji na kuziharibu, hapo ndipo walipogundua kuwa kuna wasichana wapatao mia mbili na wanawake tisini na tatu."
Kwa sasa jeshi limezuiwa kutoa utambulisho wa wasichana hao. Hata hivyo, jeshi limethibitisha kwamba wasichana hao sio wale wanafunzi waliotekwa katika mji wa Chibok.
"tuko katika mchakato wa kuwachunguza hawa wasichana ili tuweze kubaini utambulisho wao, lakini kitu kimoja nataka nikiweke wazi kwa umma, tunapotaja idadi ya wasichana mia mbili, tayari watu wanaanza kufikiria wasichana mia mbili wa Chibok waliotekwa mwaka jana, hawa sio wasichana wa Chibok, tutaendelea kuwajuza kadri muda unavyokwenda iwapo kutakuwa na taarifa zozote. "
PESA YETU INAKUFA ............ SHILINGI YA TANZANIA YAPOMROMOKA KWA % 20 DHIDI YA DOLA $
Shilingi ya Tanzania imeendelea kushuka hadi kufikia anguko la asilimia 20 dhidi ya dola ya Kimarekani,hali inayotajwa kuwa si tu inaathiri mitaji ya uwekezaji bali pia kipato cha mtu binafsi. Kwa sasa ubadilishaji wa shilingi ya Tanzania kwa dola ya Kimarekani imefikia shilingi elfu mbili kwa dola moja na kuathiri mwenendo wa kiuchumi.
MEMBE AMKUBALI LOWASSA .. AKIRI AJIRA KUA BOMU ... BADO KUKIRI LOWASSA NI JEMBE ...
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema kwamba Tanzania itaweza kufuta dhana ya wananchi wake kwenda nchi za nje kwa kuwahakikishia ajira.
Membe anasema kwamba miongoni mwa maeneo ambayo Serikali haina budi kuyaangalia kwa jicho la tatu ni kufufua viwanda na kujenga vipya badala ya kuacha wananchi wake kuanza kutafuta ajira kama hizo nje ya nchi.
..................................................................................................................................................................
MIAKA MIWILI HUKO NYUMA MBUNGE WA MONDULI NA WAZIRI MKUU MSTAAFU ALIWAHI KUTAHADHARISHA KUA TATIZO LA AJIRA NI BOMU LINALOSUBIRI KULIPUKA ..
Alipingwa na mama MUKANGARA na hawa jamaa leo AMEKUBALI KUA kweli AJIRA NI BOMU ... SAFI MEMBE pia kubali LOWASSA ni JEMBE ....
Subscribe to:
Posts (Atom)