Manny Pacquiao akiwasalimia mashabiki wake waliofika kumpokea alipowasili katika Hoteli ya Mandalay Bay jijini Las Vegas jana usiku.
Manny Pacquiao (36) na Floyd Mayweather (38) watazichapa usiku wa Jumamosi, Mei 2, mwaka huu kwenye Ukumbi wa MGM Grand uliopo Las Vegas, Marekani.
Manny alitupia picha hii katika akaunti yake ya on Instagram akiwa kwenye basi lake la kifahari wakati akielekea Las Vegas akitokea Los Angeles alipokuwa ameweka kambi.
Pacquiao akijifua kwa mara ya mwisho jijini Los Angeles kabla ya kuelekea Las Vegas.
Gari lililokuwa limembeba Manny likiwa limezingirwa na mashabiki wake nje ya ukumbi wa mazoezi huko Los Angeles wakitaka kumuaga kabla ya kuelekea Las Vegas.
Waendesha pikipiki wenye bendera za Taifa la Filipino wakilisindikiza basi lililobeba watu wa Manny kuelekea Las Vegas.
-Ataka kumchakaza Mayweather katika kila raundi
-Akataa sherehe rasmi za mapokezi yake, kuandaa sherehe yake leo kwenye hoteli
BONDIA mahiri kutoka Ufilipino, Manny Pacquiao (36) jana usiku ametua jijini Las Vegas tayari kwa pambano lake la kihistoria dhidi ya Floyd Mayweather. Pambano hilo litapigwa Mei 2, mwaka huu katika Ukumbi wa MGM Grand uliopo Las Vegas, Marekani.
Pacquiao ametua kwa basi akiambatana na wapambe wake akitokea Los Angeles umbali wa maili 270 alipokuwa akijifua.
Bondia huyo amesema anataka kumchakaza Mayweather katika kila raundi na hategemi sana kumchapa kwa knock-out (KO).
Manny pia amekataa sherehe rasmi za mapokezi yake na kusema kuwa ataandaa sherehe yake leo kwenye hoteli aliyofikia ya Mandalay Bay.
Rekodi:
Mayweather ameshinda mapambano yake yote 47, kati yake 26 ameshinda kwa knock-out (KO), kwenye miaka yake 19 ya ubondia wa kimataifa.
Pacquiao yeye ameshinda mapigano 57 kati ya 64 aliyopigana tangu alipoanza mapigano ya kimataifa mwaka 1995, kati ya hayo 38 ameshinda kwa knock-out (KO), akipoteza 5 na kutoka sare 2.
No comments:
Post a Comment