Saturday, 25 April 2015

MCHUMBA WA MWIZI AFUNGUKA .. > source G P

KWELI! Baada ya mitandao mbalimbali kuripoti habari zinazokinzana juu ya tukio la bwana harusi mtarajiwa aliyetajwa kwa jina la Stephano kunaswa kwenye tukio la ujambazi muda mfupi baada ya kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake, Happy Merere, bi. Harusi huyo mtarajiwa ameibuka na kuanika ukweli wa mambo, Risasi Jumamosi lina full stori.

Stephano akiwa na mpenzi wake, Happy Merere baada ya kumvisha pete ya uchumba.

Stephano na wenzake watatu walikamatwa Aprili 21, mwaka huu maeneo ya Red Cross jijini Dar akidaiwa kuhusika katika tukio la kumpora fedha Mzungu mmoja raia wa kigeni pale Kinondoni, Dar.
Kwenye tukio hilo, watuhumiwa hao, akiwemo Stephano au mume mtarajiwa wa Happy waliwekwa chini ya ulinzi na jeshi la polisi.


MITANDAO YAANZA

Baada ya tukio hilo kuthibitishwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na watuhumiwa Salum Mtamwa, Alex Makunga, Mohammed Ally na Stephano Kikindi kushikiliwa kwa uchunguzi zaidi, watu walianza kuripoti tofauti katika mitandao ya kijamii.Kuna ambao walidai watuhumiwa hao ni majambazi kwa vile walikutwa na bunduki mbili lakini kuna wengine walidai ni vibaka kwa kuwa hawakukutwa na silaha yoyote.


WENGINE WANADAI NDIYO TABIA YAKE

Wadau wengine kwenye mitandao ya kijamii walijiongeza kwa kudai mtuhumiwa ambaye ni mume mtarajiwa wa Happy wanamjua kwamba anajihusisha na ishu za udokozi hivyo tukio hilo si la kwanza kumtokea.


MKE MTARAJIWA AIBUKA

Risasi Jumamosi lilibahatika kuzungumza na Happy ambaye awali alianza kukanusha taarifa ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii na kudai nyingi hazina ukweli wowote, alisema:
“Wanajiandikia tu mitandaoni, hakuna ukweli wowote. Eti wanasema mchumba‘angu amekutwa na bunduki mbili wakati taarifa nilizozikuta pale Polisi Central zinasema hawakuwa na silaha.”

ASEMA SI JAMBAZI!
“Wala mchumba‘angu hakuwa jambazi kama watu walivyokuwa wanasema mitandaoni, jalada nililolikuta polisi lilikuwa limeandikwa UNYANG’ANYI na si ujambazi kama wengi walivyokuwa wanavumisha, mimi nimekwenda mwenyewe polisi nikaoneshwa.”


Stephano anayetuhumiwa kwa ujambazi.

KUMBE WAMEJUANA KITAMBO
 

Katika aya nyingine, Happy alizungumzia uhusiano wake na mumewe mtarajiwa huyo na kusema walifahamiana miaka mingi lakini hawakuwa wakiishi pamoja.“Mimi nimejuana naye miaka mingi iliyopita lakini hatukuwa tukiishi pamoja, yeye anakaa Dar, mimi nipo nyumbani kwa wazazi wangu, Iringa.”
NI MTU WA KUSAFIRI
“Hata hivyo, mimi mwenyewe nyumbani nilikuwa sikai sana, nilikuwa mtu wa kusafiri maana nina biashara zangu, hata yeye tulikuwa tunaonana mara chache.”

KAZI YA MTARAJIWA WAKE
“Tangu nimemjua mtarajiwa wangu alikuwa anafanya kazi ya ufundi wa magari pamoja na udalali wa magari, sikuwahi kusikia wala kumuona anajihusisha na wizi wa namna yoyote. Nashangaa eti watu wanadai ni mzoefu wa matukio ya wizi.”

ADAI NI MARAFIKI
“Wale watu aliokamatwa nao mchumba wangu ni marafiki zake, sasa huenda alijikuta amejumlishwa kwenye tukio ambalo halimhusu. Watu wanazungumza tu pasipo kuwa na ushahidi wowote, mimi mchumba wangu namjua sijawahi kumuona na viashiria vyovyote vya wizi,” alisema Happy.

Stephano na wenzake waliponaswa kwenye tukio hilo.
WAZAZI WACHANGANYIKIWA
Happy alizidi kuweka wazi kuwa, ameumizwa na tukio hilo kwani limewagusa wazazi wake kiasi cha kuwafanya wachanganyikiwe.“Huwezi amini, wazazi wamechanganyikiwa, wanaelezwa vitu vya uongo kuhusu mtarajiwa wangu inaniuma kwa sababu yanayoongelewa kwenye mitandao hayana ukweli, ila ngoja tusubiri vyombo vya sheria vifanye kazi yake na wote waliosema uongo wataumbuka,” alisema Happy.

TUKIO LA PETE
Februari, mwaka huu, Happy alivishwa pete na mchumba wake huyo nyumbani kwao Iringa ambapo mipango ikienda sawa, wawili hao wanatarajiwa kufunga ndoa hapo baadaye mwaka huu (Mungu akipenda).

No comments:

Post a Comment