Idadi ya watu ambao wamethibitishwa
kuaga dunia wakati kulipotokea tetemeko kubwa la ardhi nchini Nepal siku
ya Jumamosi imepanda hadi zaidi ya watu 5000.
Waziri mkuu Sushil Koirala anasema kuwa utawala unapokea maombi mengi ya kutaka msaada kutoka maeneo ya mbali ya vijiji vya Himalaya, lakini jitihada za kuyafikia maeneo hayo zinatatizwa na uhaba wa vifaa na waokoaji.
Waziri huyo mkuu anasema kuwa kuna mahitaji ya dharura ya mahema , chakula na maji. Mwandishi wa BBC aliye kwenye kijiji kuliko kitovu cha tetemeko hilo, anasema kuwa zaidi ya nusu ya nyumba katika kijiji hicho zimeharibiwa.
No comments:
Post a Comment