Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban
Ki-moon ameelezea tahadhari yake kuhusiana na hatari ya raia kuendelea
kupigana, Nchini Yemen.
Mashambulizi katika majumba ya raia zikiwemo hosptali na maghala ya vifaa vya misaa ya kibinadamu yamekuwa yakiendelea.
Kumekuwa na taarifa watu wenye silaha wamekuwa wakiwateka raia katika mitaa ya Aden.
Shirika la Umoja wa mataifa la misaada ya chakula limesema halina jinsi zaidi ya kusitisha mipango yake ya kusambaza misaada kutoka na tatizo la mafuta.
Kwa sasa mapigano makali yanaendelea katika mipaka ya eneo la Yemen na Saudia Arabia.
No comments:
Post a Comment