PSG wamvalia njuga Di Maria
*Arsenal, Man United vikumbo
matajiri wa Ufaransa, Paris St-Germain (PSG) wapo tayari kutoa pauni milioni 45 kumsajili winga wa Manchester United, Angel Di Maria.
Raia
huyu wa Argentina aliyesajiliwa kiangazi kilichopita kutoka Real Madrid
ameshindwa kuchanua kwenye Ligi Kuu ya England (EPL) na sasa PSG
wanadhani watampa raha.
Di Maria (27) aliwagharimu United pauni milioni 59.7, akivunja rekodi ya usajili nchini Uingereza lakini Kocha Louis van Gaal amemchezesha namba tofauti bila mafanikio.
Katika
mechi tano zilizopita alianzia benchi hivyo kuonekana kushindwa
kutimiza kilichotarajiwa kutoka kwake, huku familia ikiwa haina raha
baada ya wezi kujaribu kuvamia nyumba yake familia ikiwa ndani jijini
Manchester.
Wezi hao walikimbia baada ya Di Maria
kubonyeza kitufe cha kuita polisi na king’ora kulia nje ya kasri hilo.
Amehamishiwa hotelini tangu wakati huo.
Hata hivyo, Man U
wanadai hawana nia ya kumuuza winga huyu lakini PSG wanadaiwa
watawajaribu kwa kuwasilisha ofa rasmi karibuni baada ya kushindwa
kumsajili msimu uliopita.
United wanadaiwa kutia nia ya kumsajili mlinzi wa kati wa Athletic Bilbao, Aymeric Laporte, ambaye mkataba wake unasema anaweza kuuzwa ikiwa klabu inayomtaka itatoa pauni milioni 30.
Hata
hivyo Man U watakabiliana na upinzani kutoka kwa Arsenal ambao pia
wanataka kumsajili Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 21.
United wataongeza nguvu kwa chipukizi huyu iwapo mipango yao ya kumsajili mlinzi mahiri wa Borussia Dortmund, Mats Hummels.
Klabu
ya Marseille ya Ufaransa inataka kuwasiliana na Manchester City kwa
ajili ya kumchukua kocha wao wa timu ya vijana, Patrick Vieira ili awe
kocha nchini mwake kuanzia msimu ujao.
Hata hivyo, City
wanamthamini sana Vieira na si rahisi kumwachia aondoke, ambapo pia
amekuwa akifikiriwa kupewa kazi ya kocha Manuel Pellegrini iwapo bosi
huyo atafutwa kazi.
Tottenham Hotspur wanajaribu kumsajili kiungo wa Southampton, Morgan Schneiderlin, 25. Inaelezwa kwamba Saints wanataka pauni milioni 20 huku Spurs wakiwa tayari kuwapa kiungo wao, Andros Townsend, 23, au Benjamin Stambouli, 24, na kiasi kidogo cha fedha.
Spurs
na Arsenal wamekuwa wakimtaka Scheiderlin tangu msimu uliopita na
haijulikani kati ya watani hao wa kaskazini mwa London yupi atafanikiwa
safari hii, au iwapo wote watamkosa.
Arsenal, Chelsea Spurs wanapigana vikumbo kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Luton, Charlie Patino mwenye umri wa miaka 11 tu.
Bosi
wa Chelsea, Jose Mourinho amebainisha kwamba mmiliki wa klabu hiyo,
Roman Abramovich ndiye atakuwa na kauli ya mwisho juu ya hatima ya
mshambuliaji wao, Didier Drogba, 37, ambaye mkataba wake wa mwaka mmoja
unamalizika kiangazi hiki.
Newcastle wanataka kumsajili mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Vijana ya England, Patrick Bamford aliyefunga mabao 19 akiwa kwa mkopo Middlesbrough kutoka Chelsea.
Manchester United wanataka kumsajili kipa wa Spurs, Hugo Lloris, 28, ikiwa kipa wao, David De Gea, 24, atarudi nyumbani kwao Hispania kujiunga na Real Madrid.
Mshambuliaji
wa Arsenal, Theo Walcott, 26, amedai kwamba Arsenal ndio timu bora
Ulaya kwa 2015, ikiwa ni dalili kwamba hataondoka Emirates.
Mmiliki
wa Napoli, Aurelio De Laurentiis amemtaka kocha wao, Rafael Benitez
kuacha mipango ya kurudi England ili abaki na vijana wake.
Torino
wanasema huenda wakamuuza beki wao, Matteo Darmian wakipata ofa
‘kichaa’. Arsenal na Manchester United ni kati ya klabu zinazohusishwa
na mchezaji huyu wa kimataifa wa Italia.
Mshambuliaji wa
Newcastle, Adam Campbell, 21, anafanya majaribio katika klabu ya West
Bromwich Albion kwa minajili ya kusajiliwa huko.
No comments:
Post a Comment