Dustan Shekidele, Moro
Inauma sana! Mtoto mzuri wa kiume aitwaye Jumanne Mwinyimbegu,
mwenye umri wa mwaka mmoja amefariki dunia ghafla muda mfupi baada ya
kufanyiwa sherehe ya kutimiza mwaka mmoja ‘bethidei’.
Tukio
hilo la kusikitisha lilijiri nyumbani kwa wazazi wa Jumanne Mtaa wa
Saadan Kata ya Mwembesongo mkoani hapa mwishoni mwa wiki iliyopita na
kuibua simanzi nzito kwa kuwa alikuwa haumwi na ilikuwa muda mfupi baada
ya kukata keki, kulishwa na kuimbiwa ‘happy bethidei tuyuuuuu’.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa uchungu mama mzazi wa mtoto
huyo, Khadija Salum alisema: “Inaniuma sana jamani. Jumanne ni mtoto
wangu pekee ambaye ametimiza umri wa mwaka mmoja. Nikaona nimfanyie
‘bethidei’.
“Niliwashirikisha majirani zangu, cha ajabu baada ya sherehe
kukamilika majira ya saa 3:00 usiku mwanangu alijisikia uchomvu,
nikaenda kumlaza lakini hakuamka tena.
“Nimemkimbiza kwenye Zahanati ya Ngeta (Mwembesongo), nilipofika
manesi walimcheki wakaniambia mbona amekufa muda mrefu, nikarudi
nyumbani nikiwa nalia,” alisema Khadija na kuongeza:
“Baada ya uchunguzi wa madaktari ilibainika kuwa kilichomuua mwanangu
ni upungufu wa damu mwilini lakini niliwaambia alikuwa haumwi na
alifurahia bethidei vizuri na wenzake.”
Mwili wa mtoto huyo ulihifadhiwa kwenye Makaburi ya Kola huku wana
familia wakimwachia Mungu kwani kuna waliotaka kuhusisha tukio hilo na
ushirikina.
No comments:
Post a Comment