Monday, 27 April 2015

NEPAL BADO MAJONZI WALALA NJE KWA SIKU YA PILI ...>>

   

Maelfu ya raia wa Nepal wamelazimika kulala nje kwa siku ya pili mfulululizo huku barabara zilizofungwa na athari za baada ya tetemeko zikipunguza kasi ya kuwaokoa manusura.
Karibia watu 2400 wamefariki katika jenga hilo.

Makundi ya misaada yamesema kuwa kuna uhaba wa na umeme na maji huku serikali ikisema kuwa mahema zaidi na vitanda vya mda vinahitajika kwa haraka.

Mwandishi wa BBC katika mji mkuu wa Kathmandu amesema mji uliojaa waathiriwa umeibuka ambapo watu hao wanalala katika mifuko ya plastiki kwa kuwa wanahofu ya kuishi ndani ya majumba yao.

No comments:

Post a Comment