Kumetokea maandamano mapya nchini
Marekani katika mji wa Baltimore kufuatia kifo cha kijana mweusi Freddie
Gray aliyekufa kutokana na majeraha akiwa mikononi mwa polisi. Mamia ya
watu wameandamana katika mitaa, wakionyesha ujasiri licha ya hali mbaya
ya hewa iliyokuwepo.
Mtetezi wa haki za binadamu, Mchungaji Al Sharpton, ameitisha mkutano mjini Baltimore ili kuimarisha uhusiano baina ya polisi na wanajamii.
No comments:
Post a Comment