Utawala nchini Nepal unasema kuwa
watu zaidi ya watu 4000 wamedhibitishwa kuaga dunia huku wengine 8000
wakijeruhiwa kwenye janga la tetemeko la ardhi lililosababisha uharibifu
mkubwa siku ya Jumamosi.
Watu wengi walilala nje kwa usiku wa tatu mfululizo kwenye mji mkuu Kathmandu wakihofia kutokea kwa mitetemeo mingine midogo.
Serikali ya Nepal inasema kuwa inahitaji kila msaada ukiwemo wa mablanketi , helkopta, madaktari na madereva. Kuna uhaba wa maji , chakula na umeme huku kukiwa na hofu ya kutokea kwa milipuko ya magonjwa.
No comments:
Post a Comment