Mahakama ya rufaa nchini Korea
Kusini imempata na hatia ya kuua nahodha wa feri ambayo ilizama mwaka
mmoja uliopita na kumuongezea kifungo hadi cha maisha gerezani.
Jamaa za waathiriwa zililalamikia hukumu ya kwanza zikiitaja kuwa nyepesi.
Zaidi ya watu 300 wengi wao watoto walikufa wakati feri ya Sewol ilipozama. Manusura wengine walisema kuwa waliamrishwa kukaa ndani ya feri huku nahodha akiwa kati ya watu wa kwanza waliookolewa.
No comments:
Post a Comment