Monday, 27 April 2015

KWELI TWANGA PEPETA SOO... >> CHOCKY, NYAMWELA WAREJEA ‘TWANGA’ KWA MBWEMBWE, CHEREKO


Ali Chocky (katikati) akiwa na waimbaji wenzake, Luiza Mbutu (kulia), na Kalala Junior baada ya kutambulishwa.
Wanamuziki wa ‘Twanga’ wakiongozwa na Kalala Junior (kushoto) wakiwa na begi ambalo ndani yake alikuwemo mnenguaji Super Nyamwela kama moja ya staili ya kutambulishwa.
Baadhi ya wanenguaji wa bendi hiyo wakifungua begi hilo tayari kwa utambulisho wa mnenguaji mwenzao, Super Nyamwela. Nyamwela akionyesha manjonjo yake  baada ya kutambulishwa.
Wanenguaji wa kike wa bendi hiyo wakiwajibika jukwaani.
Nyamwela akiongoza safu ya wanenguaji muda mfupi baada ya kutambulishwa.
Wanenguaji wakichapa kazi jukwaani.
ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ali Chocky, na mnenguaji wake, Super Nyamwela, usiku wa kuamkia Aprili 26 walitambulishwa rasmi ndani ya ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, jijini Dar es Salaam, aliporejea bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’.  Choky ni ataendelea kuwa mmoja wa waimbaji wa bendi hiyo ambapo atafanya kazi sambamba na Luiza Mbutu na Kalala Junior.  Nyamwela ataungana na wanenguaji wengine kuimarisha safu ya wasanii wenzake.

No comments:

Post a Comment