Ligi kuu ya Tanzania Bara itaendelea
mwazoni mwa juma hili (Jumatatu) na swali pekee kwa wapenda kabumbu ni
kwamba je Yanga, iliyonzishwa mwaka 1935 itatawazwa kuwa mabingwa
wapya?. Jibu litakuwa ndio endapo vijana hao wa jangwani watawafunga
Polisi Morogoro katika mechi itakayochezwa uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Yanga, wawakilishi pekee katika ukanda wa Afrika ya
Mashariki katika michuano ya vilabu barani Afrika ambao watacheza na
Etoile du Sahel ya Tunisia mjini Tunis katika mechi ya marudiano ya
raundi ya 16 ya michuano hiyo wikiendi hii baada ya sare ya 1-1 jijini
Dar es Salaam, wana pointi 52, ambazo kimahesabu hazitaweza kufikiwa na
timu yoyote wakati ligi hiyo ikielekea ukingoni mwezi ujao.Baada ya mechi ya leo, Yanga, ikiwa chini ya kocha Mdachi, ambaye hivi karibuni ameiweka timu hiyo katika wimbi kubwa la ushindi, itabakiwa na mechi mbili tu mkononi na haina cha kupoteza hata ikifungwa kwani tayari imemuweka mwali kibindoni
Hata kama mabingwa watetezi, Azam FC, itafanikiwa kumaliza mechi zake zote za ligi, haitaweza, hata kwa miujiza kuifikia Yanga, ambayo haijashinda taji la ligi kuu kwa zaidi ya miaka 2 iliyopita
Azam, waliokuwa wawakilishi wa kombe la washindi barani Afrika (African Champions league) baada ya kutolewa katika michuano hiyo na vigogo wa Sudan, El-Merreikh, wana pointi 45 katika mechi 23 na hata kama itashinda mechi zake tatu zilizobaki, itakuwa imefikisha pointi 54, pointi moja nyuma ya Yanga kama Polisi watafungwa.
Kwa sasa vita ya nafasi ya pili ili kupata tiketi ya michuano ya kombe la Wawakilishi barani Afrika (Confederation Cup) ipo kati ya mabingwa watetezi, Azam na Simba yenye pointi 41 ikiwa na mechi mbili mkononi.
Simba, iliyonzishwa zaidi ya miaka 70 iliyopita, ikiwa chini ya kocha Mserbia, Goran Kopunovic ina Sali na kuomba du azote ili Azam iweze kuteleza katika mechi zake zilizobaki ili irudi katika chati ya michuano ya kimataifa, baada ya kuwa nje mwa miaka kadhaa.
Endapo Yanga watafanikiwa kuchukua ubingwa , wataiwakilisha Tanzania katika michuano ijayo ya kombe la Washindi barani Afrika
No comments:
Post a Comment